• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 26, 2015

  POLISI ZENJI YAAHIDI MAAJABU KOMBE LA SHIRIKISHO, YAPANIA KUPIGA WAGABON 6-0

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  LICHA ya kupoteza mchezo wao wa kwanza wa Michuano ya Kombe la Shrikisho Barani Afrika  dhidi ya CF Mounana ya Gabon kwa kufungwa mabao 5-0, maafande wa Polisi Zanzibar wameapa kuibuka na ushindi mnono na kuwatupa nje ya michuani hiyo wapinzani wao hao.
  Polisi itashuka dimbani kuikabili CF Mounana  katika pambano la marudiano litakalopigwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Amani Visiwani Unguja.

  Akizungumza na BIN ZUBEIRY, Kocha mkuu wa timu hiyo, Hamisi Sufiani alisema licha ya kufungwa katika mchezo wa awali hajawajakata tamaa na kuhakikisha wanautumia ipasavyo uwanja wa nyumbani kwa kurudisha mabao 5-0 au zaidi.
  Alisema anaamini wengi hawaamini kile  anachokisema, lakini amedhamiria kuhakikisha anawapa furaha Wazanzibar na Watatanzania kwa ujumla.
  “Mpira dakika 90, tumecheza dakika 45 na kukubali kichapo, sasa zimebaki 45 zingine ambapo tutahakikisha kufa au kupona kuhakikisha wapinzani wetu hawatoki nyumbani.
   “Kwa sasa ligi ya Zanzibar imesimamishwa lakini tangu  tumerudi kutoka Gabon hatukuvunja kambi tuliendelea na mazoezi kwaajili ya kujiandaa na mechi ya marudiano.”alisema Sufian.
  Sufiani alisema amewaandaa wachezaji wake kisaikolojia ikiwa ni pamoja na kufanyia kazi makosa madogo madogo ambayo yalijitokeza katika mchezo wa awali ambao wamefungwa bao 5-0.
  Polisi inahitaji kushinda bao 6-0 au zaidi ili kusonga mbele kwenye michuano hiyo, baada ya awali kufungwa bao 5-0 nchini Gabon wiki iliyopita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: POLISI ZENJI YAAHIDI MAAJABU KOMBE LA SHIRIKISHO, YAPANIA KUPIGA WAGABON 6-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top