• HABARI MPYA

  Jumatatu, Februari 23, 2015

  YANGA SC WALIFUATA JESHI LA BOTSWANA JUMATANO

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  KIKOSI kamili cha Yanga kinakwea pipa Jumatano alfajiri kuelekea Botsawna tayari kwa mchezo wa marudiano dhidi ya BDF XI ya huko.
  Katibu wa Yanga Dk Jonas Tiboroha amesema kikosi chao kitaondoka na wachezaji wote watakaopitishwa na kocha wao Hans Pluijm ambaye kesho atataja idadi kamili ya msafara wao.
  Tibohora ambaye pia kitaaluma  ni kocha amesema kikosi chao kitaondoka na Ndege ya Shirika la Kenya tayari kwa mchezo huo wa kombe la Shirikisho utakaopigwa Ijumaa nchini humo ambapo Yanga itarejea Jumapili baada ya mchezo huo.

  "Tunatarajia kuondoka hapa Jumatano keshokutwa kuelekea Botswana,kwasasa tunasubiri kocha na timu irejee leo ikitokea Mbeya na baada ya hapo tutamalizia maandalizi ya safari yetu,"amesema Tiboroha.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC WALIFUATA JESHI LA BOTSWANA JUMATANO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top