• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 26, 2015

  KAGERA SUGAR WAINYIMA AMANI STAND UNITED NYUMBANI KWAO

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mkuu wa Stand United ya Shinyanga, Mathias Lule ni kama ameanza kuwahofia wapinzani wake Kagera Sugar atakayokutana Jumamosi hiii kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY, Lule alisema wachezaji wa Tanzania wanalingana hivyo ni vigumu kwake kesema ana uhakika atavuna pointi tatu kwenye mchezo huo.
  “Kagera ni timu nzuri na si wakuwafungwa kirahisi kutokana na viwango vya wachezaji wa Tanzania kulingana, hivyo hufanya mchezo kuwa na ushindani wa hali ya juu,” alisema.

  Lule alisema, anachokifanya yeye kwa sasa ni kuwapa mbinu wachezaji wake ili kuhakikisha wanacheza vizuri na kupata pointi tatu  kwenye mchezo huo.
  Alisema anatarajia kuona mchezo mzuri baina ya timu hizo mbili unatoa  matokeo ya haki kutokana na malalamiko yanayotokea hivi sasa kwenye mechi mbalimbali yakiwagusa waamuzi.
  Stand ambao wapo katika nafasi ya 11 na pointi 18 kwenye msimamo wa Ligi kuu Bara, wanashuka dimbani katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu nzuri na kuwafunga Simba bao 1-0 kwenye mchezo wao uliopita.
  Ikumbukwe, Kagera Sugar japokuwa ni timu ya Bukoba mkoani Kagera, lakini imehamishia mechi zake za nyumbani Uwanja wa Kambarage, baada ya Uwanja wa Kaitaba kuingia katika zoezi la ukarabati. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR WAINYIMA AMANI STAND UNITED NYUMBANI KWAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top