• HABARI MPYA

    Sunday, February 22, 2015

    BUSARA ITUMIKE KUTATUA MGOGORO SIMBA SC, KLABU INAPOELEKEA SIKO!

    MIGOGORO ni sehemu ya maisha ya kila siku ya klabu kongwe nchini za Simba na Yanga na watafiti wa mambo wanaamini huwa ni chokochoko za watu maalum kwa maslahi yao binfasi.
    Inakuwa vigumu kuamini hata huu mgogoro unaoendelea hivi sasa Smba SC umepandikizwa, kutokana na historia yake.
    Usipozama ndani unaweza kuamini mgogoro huu unaanzia wakati wa uchaguzi uliopita wa klabu hiyo Mei mwaka jana, ambao ulimuweka madarakani, Evans Aveva kuwa Rais wa klabu.
    Ukweli ni kwamba mgogoro huu ni matokeo ya makovu ya migogoro ya tangu wakati wa uongozi wa marehemu Juma Salum Muhovuge.

    Makundi yaliyozaliwa wakati huo, yameendelea kuigawa klabu hiyo hadi sasa na mbaya zaidi, hakuna dalili za kufikiwa mwafaka, zaidi ya mambo kutulizwa tu.
    Matokeo mazuri ya timu wakati fulani yalileta utulivu au maarifa mengine, lakini ukweli ni kwamba Simba SC haijawa shwari kwa takriban miaka 10 sasa.
    Hassan Daalal hakuwa na amani madarakani wakati wake, kadhalika na Ismail Aden Rage pia.
    Na unaweza kuona hata sasa, Aveva hana amani madarakani- licha ya jitihada za wazi za kuleta mabadiliko katika klabu kwa pamoja na washirika wake, Friends Of Simba.
    Hakuna haja ya kupindisha maneno kumpa faida mtu, wakati klabu inazidi kudorora.
    Wana Simba SC hawajui ladha ya michuano ya Afrika kwa mwaka wa tatu sasa na bado watu wanataka kutumia ujanja ujanja tu wa kutuliza mambo, badala ya kuelekeza nguvu kwenye tatizo halisi.
    Yanga SC na Azam FC wanapishana pale kileleni mwa Ligi Kuu, wakati Simba SC inajivuta vuta na dalili zimekwishaanza kuonekana kwa mara nyingine, Wekundu wa Msimbazi hawatakuwa na chao msimu huu pia.
    Hii ni kero kwa mashabiki na wapenzi wa timu hiyo- kwa sababu wanataka ubingwa wa Ligi Kuu na kurudi kucheza mashindano ya Afrika- na si hivi vikombe vya Banc ABC, Mapinduzi na Saleh Hijja pekee.
    Katika makala yangu iliyopita niliandika wazi kwamba, kauli mbiu ya Simba SC iliyowekwa na waasisi wa klabu ni “Nguvu Moja”, hivyo kama klabu inakuwa na makundi, matabaka inapoteza maana yake halisi.
    Tunataka umoja urejeshwe ndani ya Simba SC. Kipi kinashindikana? 
    Uongozi wa Simba SC unapaswa kujitambua wao ndiyo kama mzazi, wa watoto ambao ni wanachama na wapenzi wa klabu.
    Kama imetokea wanachama wamekosea, kitendo cha uongozi kuendelea kupambana na kushindana nao, hakisaidii zaidi ya kuzidi kuiumiza klabu.
    Uongozi wa Simba SC unataka wanachama walio ‘msituni’ maarufu kama ‘Simba Ukawa’, wakafute kwanza kesi waliyofungua mahakamani ndiyo watambuliwe.
    Ukawa nao hawataki hilo, wameendelea kuwa msituni kiasi cha kuunyima raha uongozi uliopo madarakani.
    Ukweli ni huo, uongozi wa Aveva hauna raha madarakani, ndiyo maana wanahangaika na Ukawa, mara wawakamate na ndumba, mara wawatuhumu kuhujumu timu na kadhalika.
    Kama kungekuwa kuna umoja ndani ya klabu, haya yote yasingekuwa yanatokea.  Msimamo wa uongozi kutaka kwanza Ukawa wafute kesi ni mgumu kutekelezeka, kwa sababu hiyo ndiyo silaha ya wapinzani wao.
    Kama Ukawa watafuta kesi, watausumbua kwa lipi lingine uongozi wa Aveva. Hapa lazima busara itumike kwa kutanguliza mbele maslahi ya Simba SC.
    Lazima pande mbili zinazopingana zikutanishwe na makubaliano ya msingi ya kurejesha amani na umoja klabuni yafikiwe.
    Kama uongozi wa SImba SC bado hautooona umuhiumu wa kufanhya hivyo, ujue kwamba unazidi kjuchocha moto klabuni kwao.
    Hakyumkiniki uongozi kushindana na wanachama wake, badala ya kutafuta sukuhisho la matayizo ndani ya klabu,
    Kamati ya Utendaji ya SImba SC cbhini ya Rais Avevam inapaswa kuongoza klabu kwa amani bila mawazo, ya nani anahujumu timu, nani analoga. Ndiyo maana ninasema, busara itumike kurehesa maani na umoja SImba SC. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BUSARA ITUMIKE KUTATUA MGOGORO SIMBA SC, KLABU INAPOELEKEA SIKO! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top