• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 26, 2015

  YANGA SC YAMTIMUA MWANAJESHI WA BOTSWANA ALIYEVAMIA KAMBI YAO

  Na Mwandishi Wetu, GABORONE
  KLABU ya Yanga imefanikiwa kumnasa mmoja wa mashushu wa wapinzani wao BDF ya Botswana baada ya kumbaini mmoja wa maofisa wakubwa wa jeshi akiweka kambi katika hoteli yao.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY leo, Mkuu wa msafara wa Yanga ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ayoub Nyenzi amesema kiongozi huyo wa jeshi aliyejitambulisha kwao kwa cheo cha kanali alikuwa kambini hapo katika hoteli ya Oasis tangu jana kabla ya leo kushtukiwa.

  Sajini wa jeshi la Botswana, Omphile Machongo akiwa ameshika nyoka katika hifadhi ya Jeshi la nchi hiyo, Snake Park hivi karibuni. Askari mmoja wa jeshi la nchi hiyo (jina halikugfahamika) ametimuliwa katika kambi ya Yanga SC mjini Gaborone

  Nyenzi amesema baada ya kumabini kiongozi huyo akishirikiana na wenzake ambao ni katibu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha na Mkuu wa mawasiliano wa timu hiyo Jerry Muro bosi huyo ambaye kila wakati wa kula alikuwa akizunguka katika sehemu ya timu yao wakati wakipata msosi walilazimika kuzungumza naye na kumwambia hatakiwi hapo kwa kuwa tayari walishakabidhiwa mwenyeji wao.
  "Tunajua kanuni za Caf kuna mtu alishatambulishwa kwetu tangu tunafika hapa jana sasa huyu mzee jana alikuwa hapa tukajua ataondoka lakini leo asubuhi tena tumemuona  tukaona hapana ngoja tuchukue tahadhari kwa kumuuliza maswali na kumwambia aondoke,"amesema Nyenzi. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC YAMTIMUA MWANAJESHI WA BOTSWANA ALIYEVAMIA KAMBI YAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top