• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 21, 2015

  MTIBWA SUGAR WAPO MKWAKWANI NA MIGAMBO JIONI YA LEO

  Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
  LIGI Kuu ya Vodacom inaendelea leo (Jumamosi)  katika viwanja vitatu tofauti, Mgambo Shooting watakua wenyeji wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
  Ndanda FC ya Mtwara watawakaribisha Wagosi wa Kaya timu ya Coastal Union kutoka jijini Tanga katika mchezo utakaochezwa kwenye dimba la Ngwanda Sijaona.
  Huku wakata miwa wa Kagera Sugar wanaoutimia Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga wakiwakaribisha Maafande wa Jeshi la Polisi kutoka mjini Morogoro timu ya Polisi.

  Ligi hiyo ya Vodacom itaendelea tena kesho jumapili katika viwanja vitatu   tofauti, Uwanja wa Chamazi wenyeji Azam FC wataikaribisha timu ya maafande wa Jeshi la Magereza nchini Tanzania Prisons, mchezo utakaonza majira ya saa 2 kamili usiku.
  Mjini Shinyanga wenyeji timu ya Stand United wataikaribisha Simba SC kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, huku wagonga nyundo wa jiji la Mbeya, timu ya Mbeya City wakicheza na timu ya Young Africans kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR WAPO MKWAKWANI NA MIGAMBO JIONI YA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top