• HABARI MPYA

  Ijumaa, Februari 20, 2015

  MSUVA AFIKISHA MABAO 24 YANGA SC

  Na Prince Akbar, MBEYA
  WINGA wa Yanga SC, Simon Msuva jana amefunga bao lake 24 tangu amejiunga na klabu hiyo mwaka 2012 akitokea Moro United.
  Simon alifunga mabao mawili katika ushindi wa 3-0 jana wa Yanga SC dhidi ya wenyeji Prisons Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  Na kwa ushindi huo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC inapanda kileleni kwa kutimiza pointi 28 baada ya kucheza mechi 14, hivyo kuwazidi kwa pointi mbili mabingwa watetezi, Azam FC.
  Simon Msuva akishangilia baada ya kufunga bao lake la 24 jana tangu ajiunge na Yanga SC mwaka 2012
  Andrey Coutinho ndiye alikuwa mpishi wa mabao yote ya Yanga SC jana
  Wachezaji wa Yanga SC wakiwapongeza Msuva na Coutinho jana Sokoine

  Mabao yote ya Msuva jana yalitokana na kona maridadi za kiungo Mbrazil, Andrey Coutinho ambaye pia alisababisha na bao la tatu. Coutinho alipiga shuti ambalo lilimbabatiza beki wa Prisons, Lugano Mwangama na kutinga nyavuni. 
  Tangu amejiunga na Yanga SC, akisajiliwa kama mchezaji wa timu ya vijana kutoka Moro United, Msuva amekwishaichezea timu hiyo mechi 
  86.
  Mabao ya Msuva jana, yalifuta ukame wa mabao wa kinda huyo uliodumu tangu Januari- kwani kwa kipindi chote hicho imeshuhudiwa akikosa mabao ya wazi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MSUVA AFIKISHA MABAO 24 YANGA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top