• HABARI MPYA

  Ijumaa, Februari 20, 2015

  BALOTELLI AING’ARISHA LIVERPOOL ULAYA, APORA MPIRA NA KWENDA KUPIGA PENALTI YA USHINDI ANFIELD

  BAO pekee la mshambuliaji wa kimataifa wa Italia, 
  Mario Balotelli limeipa Liverpool ushindi wa 1-0 dhidi ya Besiktas katika mchezo wa kwanza hatua ya 32 Bora Europa League Uwanja wa Anfield usiku huu.
  Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester City, Inter Milan na AC Milan, alifunga bao hilo kwa penalti dakika ya 85, kufuatia winga Jordon Ibe kuchezewa faulo kwenye eneo la hatari.
  Mtaliano huyo alimpokonya mpira Nahodha Jordan Henderson na ‘akazinguana’ na Daniel Sturridge kabla ya kwenda kupiga.
  Mapema, Demba Ba na Adam Lallana walipoteza nafasi nzuri za kufunga kwa kila timu na baada ya ushindi huo mwembamba Anfield, Liverpool inajiweka katika mazingira magumu kuelekea mchezo wa marudiano nchini Uturuki Alhamisi ijayo.
  Kikosi cha Liverpool kilikuwa; Mignolet, Can, Skrtel, Sakho, Ibe, Henderson, Allen/Lovren dk63, Moreno, Lallana/Sterling dk77, Sturridge na Coutinho/Balotelli dk63.
  Besiktas: Gonen, Kurtulus, Franco, Gulum, Ramon, Hutchinson, Kavlak, Tore, Sosa/Ozyakup dk60, Sahan/Frei dk72 na Ba.
  Balotelli celebrates in front of the Liverpool fans after converting from the spot to give his side a narrow victory
  Balotelli akishangilia 'kigumu' mbele ya mashabiki wa Liverpool baada ya kufunga 

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2960677/Liverpool-1-0-Besiktas-Substitute-Mario-Balotelli-scores-late-penalty-Reds-edge-narrow-victory-leg-Anfield.html#ixzz3SFJIVx8i 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BALOTELLI AING’ARISHA LIVERPOOL ULAYA, APORA MPIRA NA KWENDA KUPIGA PENALTI YA USHINDI ANFIELD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top