• HABARI MPYA

    Thursday, November 06, 2014

    YAYA TOURE AWAOMBA RADHI MAN CITY KWA KADI NYEKUNDU

    MWANASOKA bora wa Afrika, Yaya Toure amewaomba radhi wapenzi wa Manchester City kwa kadi nyekundu aliyopewa jana kwenye mechi na CSKA Moscow, wakifungwa 2-1.
    Toure alikuwa mchezaji wa pili wa City kutolewa nje katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Etihad, kufuatia Fernandinho kutolewa mapema.
    Nyota huyo wa Ivory Coast aliifungia timu ya Manuel Pellegrini bao la kusawazisha kwa mpira wa adhabu, kabla ya Seydou Doumbia kufunga kwa mara ya pili, kuipatia timu ya Urusi bao la ushindi. 
    Yaya Toure akionyeshwa kadi nyekundu kwa kumsukuma Alekseevich Eremenko kipindi cha pili

    Toure ametweet: "Mashabiki wa City- Samahani kwa kadi yangu nyekundu. Nafikiri ni muhimu kuomba radhi kwa hili,".
    Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31, awali alitweet: "Siku ya Mchezo... #Fuatilia'.
    City sasa inashika mkia kwenye kundi katika kuwania kucheza hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa na Pellegrini lazima ashinde dhidi ya Bayern Munich nyumbani kabla ya kwenda kupambana ugenini na Rome katika mchezo wa mwisho.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YAYA TOURE AWAOMBA RADHI MAN CITY KWA KADI NYEKUNDU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top