• HABARI MPYA

    Thursday, November 06, 2014

    CECAFA YAIOMBA SUDAN KUANDAA CHALLENGE BAADA YA ETHIOPIA KUPIGA CHINI

    Na Mwandishi Wetu, NAIROBI
    BARAZA la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limeiomba Sudan kuwa mwenyeji wa Kombe la Challenge mwaka huu, michuano iliyopangwa kuanza Novemba.
    Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye amsema kwamba, Shirikisho la Soka la Sudan linatarajiwa kutoa majibu kabla ya mwishoni mwa wiki.
    Pamoja na hayo, amesema hakuna nafasi ya nchi nyingine kuomba uenyeji wa michuano hiyo baada ya Ethiopia kujitoa.
    Katibu wa CECAFA, Nicholas Musonye

    “Tumewaomba Sudan kuandaa. Tumewaandikia na tunasubiri majibu yao, uwezekano kabla ya mwishoni mwa wiki,” amesema Musonye alipozunumza na futaa.com ya Kenya.
    Sudan ilifika Fainali katika michuano hiyo ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati mwaka jana na kufungwa 2-0 na wenyeji, Kenya, shukrani kwake Allan Wanga aliyefunga mabao yote. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CECAFA YAIOMBA SUDAN KUANDAA CHALLENGE BAADA YA ETHIOPIA KUPIGA CHINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top