Friends Rangers (pichani) imetoka sare ya kufungana bao 1-1 na Polisi Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Karume, Dar es Salaam. Magige Bellence alitangulia kuifungia Polisi dakika ya 67, kabla ya Friends kusawazisha dakika ya 88 kupitia kwa Almasi Mkinda, aliyefunga kwa penalti, baada ya Salmin Mohamed kuunawa mpira. Friends inatimiza pointi 12 sawa na Majimaji ya Songea inayoongoza Kundi A. |
0 comments:
Post a Comment