• HABARI MPYA

    Monday, November 03, 2014

    MBEYA CITY YAPIGWA 2-1 NA MGAMBO, SASA YASHIKA MKIA LIGI KUU…KWELI TEMBO UKILISIFIA

    Na Oscar Assenga, TANGA
    MBEYA City imeendelea kufanya vibaya katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya jioni ya leo kufungwa mabao 2-1 na Mgambo JKT Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
    Kwa matokeo hayo, Mbeya City inabaki mkiani mwa Ligi Kuu baada ya kuambulia pointi tano katika mechi sita, maana yake iko hatarini kushuka daraja. 
    Kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi
    yupo katika wakati mgumu
    Malimi Busungu aliifungia bao la kwanza Mgambo JKT dakika ya 11 kwa penalti kufuatia Nassor Gumbo kukwatuliwa na Hassan Mwasapili katika eneo la hatari na refa Israel Nkongo wa Dar es Salaam akatoa adhabu hiyo.
    Mgambo ambayo wikiendi hii itacheza na Yanga SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ilipata bao lake la pili dakika ya 24 kupitia kwa Ally Nassor, kabla ya kiungo wa zamani wa Simba SC, Steven Mazanda kuifungia bao la kufutia machozi dakika ya 76.
    Mbeya City ilikuwa timu tishio msimu uliopita baada ya kupanda tu Ligi Kuu, kiasi cha kumaliza katika nafasi ya tatu, nyuma ya Yanga SC na Azam FC, lakini msimu huu imepoteza makali. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MBEYA CITY YAPIGWA 2-1 NA MGAMBO, SASA YASHIKA MKIA LIGI KUU…KWELI TEMBO UKILISIFIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top