• HABARI MPYA

    Monday, November 03, 2014

    ARSENAL KUMKOSA WILSHERE KESHO LIGI YA MABINGWA, RAMSEY NAYE...

    KIUNGO wa Arsenal, Jack Wilshere ataukosa mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Anderlecht katakana na kuwa mgonjwa, lakini Arsene Wenger amesema mchezaji huyo atakuwa fiti kwa mchezo wa Jumapili na Swansea.
    Wilshere, ambaye anasumbuliwa na maumivu ya goti, hakufanya mazoezi leo, lakini aliripoti makao makuu ya klabu, viwanja vya Colney, London. 
    Wenger pia amesema kwamba Aaron Ramsey, ambaye amekuwa fiti tena, amekuwa pia akisumbuliwa na maradhi siku chache zilizopita- lakini kocha wa The Gunners amesema naye hatakuwa nje kwa muda mrefu.

    Jack Wilshere hakufanya mazoezi leo na Arsenal kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Anderlecht Jumanne
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARSENAL KUMKOSA WILSHERE KESHO LIGI YA MABINGWA, RAMSEY NAYE... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top