Na Theonist Buberwa, DAR ES SALAAM
HABARI kwamba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilinunua magari mawili hewa, ni uzushi wenye lengo kulipaka matokeo shirikisho hilo, chini ya rais wake, Jamal Malinzi.
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi umebaini kuwa ni kweli uongozi wa Malinzi baada ya kuingia madarakani Oktoba mwaka jana, ulinunua mabasi mawili mapya ili kuongeza ufanisi katika utendaji.
Kabla ya hapo, TFF ilikuwa ina mabasi mawili tu, moja kubwa na lingine dogo, ambayo yote yalitolewa na wadhamini wa timu ya taifa, Taifa Stars, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Lakini mabasi hayo mawili, yalikuwa hayakidhi mahitaji ya timu za taifa, kuanzia U15, U17, U20, U23 ya wakubwa na wanawake, ambazo zote zimekuwa zikishiriki mashindano.
TFF ikaona bora japo kununua mabasi mengine madogo mawili, aina ya Hiece kwa matumizi ya timu za vijana na wanawake.
Mabasi yaliyonunuliwa na TFF yana namba za usajili T511 CRB na T917 CUG na magari yote hayo yamesajiliwa kama mali ya shirikisho kwa mujibu wa kadi zake za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ambazo mwandishi amefanikiwa kupata nakala zake.
Kununuliwa kwa mabasi hayo kumekwenda sambamba na ongezeko la ajira za madereva kwa ajili ya kuyaendesha na mmoja wa walionufaika na ajira hizo ni mchezaji wa zamani wa timu ya taifa, Ally Ruvu.
Katika siku za karibuni kumekuwa na mfululizo wa habari za upotoshaji kuhusu TFF, ambazo uchunguzi wa mwandishi umebaini nyingi ni zinatokana na chuki dhidi ya Malinzi na hazina ukweli wowote ndani yake.
Malinzi amejikuta katika wakati mgumu tangu aingie TFF kutokana na kujengewa chuki na ‘wadau’ baada ya kuziba mianya ya watu kujivunia mamilioni ya ‘bure’ kwa tenda za ‘longolongo’.
Wafanyabiashara ambao walikuwa wana tenda za kujivunia mamilioni ya ‘ubwete’ wameamua kuingia msituni kupambana na Malinzi kumvuruga katika uongozi wake ili ashindwe na kuna wakati ziliibuka tuhuma kwamba walifikia hadi kuhujumu Taifa Stars.
Pamoja na hayo, Malinzi ameonyesha ukomavu wa hali ya juu kwa kuendelea na utendaji wake wa kila siku juu ya mikakati ya kuikwamua soka ya Tanzania pasipo kujali chuki hizo.

![]() |
Haya ndiyo mabasi ambayo uongozi mpya wa TFF chini ya Rais, Jamal Malinzi ulinunua baada ya kuingia madarakani |
Mabasi yaliyonunuliwa na TFF yana namba za usajili T511 CRB na T917 CUG na magari yote hayo yamesajiliwa kama mali ya shirikisho kwa mujibu wa kadi zake za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ambazo mwandishi amefanikiwa kupata nakala zake.
Kununuliwa kwa mabasi hayo kumekwenda sambamba na ongezeko la ajira za madereva kwa ajili ya kuyaendesha na mmoja wa walionufaika na ajira hizo ni mchezaji wa zamani wa timu ya taifa, Ally Ruvu.
Katika siku za karibuni kumekuwa na mfululizo wa habari za upotoshaji kuhusu TFF, ambazo uchunguzi wa mwandishi umebaini nyingi ni zinatokana na chuki dhidi ya Malinzi na hazina ukweli wowote ndani yake.
Malinzi amejikuta katika wakati mgumu tangu aingie TFF kutokana na kujengewa chuki na ‘wadau’ baada ya kuziba mianya ya watu kujivunia mamilioni ya ‘bure’ kwa tenda za ‘longolongo’.
![]() |
Kadi za usajili wa magari hayo, zikionyesha ni mali ya TFF |
Wafanyabiashara ambao walikuwa wana tenda za kujivunia mamilioni ya ‘ubwete’ wameamua kuingia msituni kupambana na Malinzi kumvuruga katika uongozi wake ili ashindwe na kuna wakati ziliibuka tuhuma kwamba walifikia hadi kuhujumu Taifa Stars.
Pamoja na hayo, Malinzi ameonyesha ukomavu wa hali ya juu kwa kuendelea na utendaji wake wa kila siku juu ya mikakati ya kuikwamua soka ya Tanzania pasipo kujali chuki hizo.
0 comments:
Post a Comment