• HABARI MPYA

    Thursday, November 06, 2014

    MRISHO NGASSA AWEKA REKODI AFRIKA, MTANZANIA WA KWANZA KUWA MFUNGAJI BORA LIGI YA MABINGWA

    MSHAMBULIAJI wa Yanga SC, Mrisho Khalfan Ngassa ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Tanzania kuwa mfungaji bora wa michuano ya Afrika, baada ya kumaliza na mabao sita katika Ligi ya Mabingwa Afrka, ingawa timu yake haikufika hatua ya makundi.
    Ngassa amefungana na Haythem Jouini wa Esperance ya Tunisia, Firmin Ndombe Mubele wa AS Vita ra DRC iliyofika fainali na El Hedi Belameiri wa Es Setif iliyoibuka bingwa kwa kufunga mabao sita kila mmoja.
    Ngassa aliifungia Yanga SC mabao yote hayo katika hatua ya awali dhidi ya Komorozine ya Comoro kabla ya kutolewa na Ahly ya Misri katika hatua iliyofuata. Ahly nayo ilitolewa pia na kuangukia kwenye Kombe la Shiriksho, ambako imefika Fainali.  
    Hongera; Mrisho Ngassa amefungana na wachezaji wengine watatu katika ufungaji bora Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu

    ORODHA YA WAFUNGAJI BORA LIGI YA MABINGWA AFRIKA TANGU 2004


    MSIMUMFUNGAJI BORATIMUMABAO
    2014TanzaniaMrisho Ngasa6
    TunisiaHaythem JouiniEspérance TunisEspérance Tunis6
    Congo DRFirmin Ndombe Mubele6
    FranceEl Hedi Belameiri6
    2012GhanaEmmanuel ClotteyEspérance TunisEspérance Tunis12
    2011ZimbabweEdward SadombaAl-Hilal OmdurmanAl-Hilal Omdurman7
    2010NigeriaMichael EneramoEspérance TunisEspérance Tunis8
    2009Congo DRDioko KaluyitukaTP MazembeTP Mazembe8
    2008NigeriaStephen WorguEnyimba AbaEnyimba Aba13
    2007Congo DRTrésor MputuTP MazembeTP Mazembe9
    2006EgyptMohamed Abou-TreikaAl-AhlyAl-Ahly8
    2005EgyptMohamed BarakatAl-AhlyAl-Ahly7
    2004SenegalMamadou DialloPahang FAPahang FA10
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MRISHO NGASSA AWEKA REKODI AFRIKA, MTANZANIA WA KWANZA KUWA MFUNGAJI BORA LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top