MABAO ya ugenini mwaka huu yatabakia kwenye kumbukumbu mbaya za watu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Hiyo inafuataia AS Vita kulikosa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kuzidiwa kete Entente Setif ya Algeria.
Setif imetwaa taji la pili la Ligi ya Mabingwa kufuatia sare ya 1-1 usiku wa kuamkia jana na AS Vita Uwanja wa Stade Mustapha Tchaker mjini Younes akitangulia kuwafungia wenyeji dakika ya 49 kabla ya Mabidi kuisawazishia Vita dakika ya 54. 

Matokeo hayo yanafanya sare ya jumla ya 3-3 baada ya awali timu hizo kutoka 2-2 mjini Kinshasa na Black Eagles wanaangushwa na mabao ya ugenini.
Hilo na taji la kwanza kwa Setif tangu mwaka 1988 na kwa klabu za Algeria ni la kwanza tangu mwaka 1990. TP Mazembe ilitolewa na Setif pia katika Nusu Fainali kwa mabao ya ugenini, ikifungwa 2-1 ugenini na kushinda 3-2 nyumbani.
Kikosi cha Etente Setif kilikuwa; Khedairia; Lagraa, Mellouli, Demmou, Megatli, Zerara, Ze Ondo, Djahnit/Mohamed dk83, Belameiri/Lamri dk80, Ziaya/Benyettou dk67 na Younes.
AS Vita: Lukong; Mabele, Dayo, Mouegni, Simbi, Llusadisu/Kanda dk74, Mabidi, Omba, Mubele, Luvumbu na Sentamu/Kasereka dk90+2.
0 comments:
Post a Comment