• HABARI MPYA

    Monday, November 03, 2014

    OKWI KUFANYIWA VIPIMO LEO, SIMBA SC WAENDA UFUKWENI KUSAKA UPEPO

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI wa Simba SC ya Dar es Salaam, Mganda Emmanuel Okwi leo atafanyiwa vipimo kujua anaendeleaje na maumivu yake ya kifundo cha mguu, imeelezwa.
    Mchezaji huyo wa zamani wa SC Villa ya Uganda, Etoile du Sahel ya Tunisia na Yanga SC ya Dar es Salaam, alitonesha enka yake katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Mtibwa Sugar.
    Okwi alitolewa kipindi cha pili katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodavom Tanzania Bara ambao timu hizo zilitoka sare ya 1-1 na Dk Yassin Gembe wa Simba SC amesema leo atampima mchezaji huyo.
    “Baada ya mechi ya Jumamosi wachezaji walikuwa wana mapumziko na tunatarajia leo tutakutana tena kwa ajili ya mazoezi na nitatumia fursa hiyo kuwafanyia vipimo wachezaji wote ambao walipata maumivu katika mchezo huo,”amesema.
    Gembe amesema mbali na Okwi, kiungo Awadh Juma naye aliumia misuli kidogo wakati mshambuliaji Elias Maguri aliumia nyama. “Ila maumivu yote ambayo walipata hawa wachezaji hayakuwa makubwa ni kidogo tu, lakini leo nitajua zaidi,”amesema.
    Dk Yassin Gembe akimtoa nje Okwi kumpatia tiba Jumamosi Uwanja wa Jamhuri

    Jioni ya leo, Simba SC watafanya mazoezi kwenye ufukwe wa Coco Beach mjini Dar es Salaam kabla ya kuendelea na programu nyingine kesho.
    Baada ya sare hiyo ya sita mfululizo tangu kuanza kwa ligi, Simba SC itashuka tena dimbani wikiendi hii kumenyana na Ruvu Shooting katika mfululizo wa Ligi Kuu ikijaribu kusaka ushindi wa kwanza. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: OKWI KUFANYIWA VIPIMO LEO, SIMBA SC WAENDA UFUKWENI KUSAKA UPEPO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top