KOCHA Louis van Gaal amemuita Chris Smalling ‘pumbavu’ kwa kujiruhusu kutolewa nje katika katika mechi dhidi ya mahasimu wa Jiji la Manchester, Man City ambayo United ilipoteza na kujikuta katika mwanzo mbaya zaidi ndani ya misimu 28.
Sergio Aguero aliifungia bao pekee City dakika ya 63 kwenye ushindi huo wa 1-0 lakini kosa hilo lilitangulia dakika sita kabla wakati Smalling alipomkwatua James Milner na kupewa kadi ya pili ya njano na refa Michael Oliver, baada ya awali kupewa pia njano kwa kumchezea rafu kipa Joe Hart.
"Katika mechi ya mahasimu unatakiwa kuwa makini — kadi ya pili ya njano ni kadi ya njano ya kipumbavu,’ amesema Van Gaal. "Ya kwanza sikuona, lakini kama mchezaji ukiwa na ya njano, unatakiwa kuifanyia kazi. Unatakiwa kujidhibiti katika mchezo wake. Nawaambia hivi wachezaji,"
0 comments:
Post a Comment