• HABARI MPYA

    Tuesday, November 11, 2014

    CAF YAIVUA RASMI MOROCCO UENYEJI WA AFCON, MRITHI WAKE KUTAJWA MARA MOJA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeivua rasmi Morocco uenyeji wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika leo Jumanne na sasa imeingia rasmi kwenye mchakato wa kusaka nchi mbadala.
    Aidha, CAF pia imeiengua Morocco kucheza Fainali hizo ambazo imesema itafanyika kama ilivyopangwa kuanzia Januari 17 hadi February 8, mwakani.
    Morocco imevuliwa uenyeji wa michuano hiyo baada ya ombi lake la kutaka isogezwe mbele kwa kuhofia ugonjwa wa Ebola kukataliwa.
    Morocco inaamini maelfu ya wasafiri kutoka Magharibi mwa Afrika wanakabiliwa na hatari ya maambukizi ya ugonjwa wa Ebola na wakataka michuano hiyo isogezwe mbele kwa angalau miezi sita huku vita dhidi ya ugonjwa huo ikiendelea.
    Lakini CAF ilikataa ombi hilo na kuipa Morocco hadi Jumamosi kuwa imeondoa ombi lake.
    CAF imesema imepokea maombi ya nchi kadhaa zilizo tayari kuipokea Morocco uenyeji wa michuano hiyo kwa mujibu wa kalenda yake, lakini haijataja nchi hata moja. Hakuna nchi hata moja iliyoonyesha nia yake hadharani yake ya kuandaa michuano hiyo.
    CAF imesema sasa itapitia maombi hayo na kutaja nchi mpya itakayobahatika kupewa uenyeji wa AFCON ya mwakani, ingawa haikutaja muda maalum wa kukamilisha zoezi hilo.
    Pia watataja tarehe na mahala ambako droo ya michuano hiyo itafanyika, badala ya mjini Rabat, Morocco ilipokuwa ifanyike Novemba 26.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CAF YAIVUA RASMI MOROCCO UENYEJI WA AFCON, MRITHI WAKE KUTAJWA MARA MOJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top