• HABARI MPYA

    Sunday, November 02, 2014

    ASHANTI UNITED YAENDELEA KUWA 'ASUSA' DARAJA LA KWANZA

    ASHANTI United imeendelea kuboronga katika Ligi Daraja la Kwanza, baada ya leo kufungwa 1-0 na Tessema katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
    Hicho kinakuwa kipigo cha pili mfululizo kwa Ashanti ya Ilala, baada ya kufungwa 2-1 na Friends Rangers katika mchezo uliopita Uwanja huo huo.
    Mechi nyingine za ligi hiyo leo, Kurugenzi imelazimishwa sare ya 1-1 na Majimaji ya Songea, Lipuli imeifunga 1-0 Kimondo Uwanja wa Samora mjini Iringa Geita imechapwa 2-1 nyumbani na Polisi Tabora, wakati Polisi Mara imefungwa 1-0 nyumbani na JKT Oljoro.  
    Ashanti United imeendelea kugawa pointi Ligi Daraja la Kwanza
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ASHANTI UNITED YAENDELEA KUWA 'ASUSA' DARAJA LA KWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top