• HABARI MPYA

    Tuesday, October 14, 2014

    UHOLANZI 'FULL MUZIKI' WAOIGWA 2-0 NA ICELAND, HIDDINK MAMBO MAGUMU MECHI NNE KAFUNGWA TATU

    UHOLANZI ikiwa imekamilika imechapwa mabao 2-0 na Iceland katika mchezo wa Kundi A kufuzu Euro 2016 usiku wa jana.
    Huo unakuwa mchezo wa tatu katika mechi nne Uholanzi inafungwa tangu ianze kufundishwa na Guus Hiddink aliyechukua nafasi ya Louis Van Gaal aliyehamia Manchester United baada ya Kombe la Dunia.
    Mabao ya Iceland jana yalifungwa na Gylfi Sigurdsson dakika ya 10 kwa penalti na 42- na sasa wanakabana koo kileleni mwa Kundi hilo na Jamhuri ya Cezch.
    Katika mchezo mwingine wa kundi hilo, Czech imeifunga 4-2 Kazakhstan mabao yake yakitiwa ‘kwenye kamba’ na Boreck Dokal dakika ya 13, David Lafata dakika ya 44, Ladislav Krejci dakika ya 56 na Tomas Necid dakika ya 88, wakati ya wenyeji yalifungwa na Yuri Yogvinenko dakika ya 84 na 90.
    Latvia imetoka sare ya 1-1 na Uturuki. Bao la Latvia iliyomaliza pungufu baada ya Gints Friemanis kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 90, lilifungwa na Valerijs Sabala kwa penalti dakika ya 54 wakati la Uturuki limefungwa na Bilal Kisa dakika ya 47.  
    Kikosi cha Uholanzi kilichoanza jana na kuchapwa 2-0
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UHOLANZI 'FULL MUZIKI' WAOIGWA 2-0 NA ICELAND, HIDDINK MAMBO MAGUMU MECHI NNE KAFUNGWA TATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top