• HABARI MPYA

    Tuesday, October 14, 2014

    ITALIA YASHINDA 1-0 KUFUZU EURO, ILA CROATIA WAMEFANYA BALAA...WAMEMTANDIKA MTU 6-0

    BAO pekee la Graziano Pelle dakika ya 24, limeipa Italia ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya Malta katika mchezo wa Kundi H kufuzu Euro 2016 usku wa jana.
    Malta ilimaliza pungufu baada ya Nahodha wake, Michael Mifsud kutolewa kwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Alessandro Florenzi. Mchezo mwingine wa Kundi hilo, Croatia imeilaza Azerbaijan 6-0 mabao yake yakifungwa na Andrej Kramaric, Ivan Parisic mawili, Marcelo Brozovic na Luka Modric wakati lingine Sadygov alijifunga.
    Norway imeifunga Bulgaria 2-1, mabao yake yakitiwa nyavuni na Elyounoussi dakika ya 13 na Haavard Nielsen dakika ya 72, wakati la wapinzani wao limefungwa na Nikolay Bodurov dakika ya 43.

    Pelle akiruka juu kuopoga kichwa dhidi ya mabeki wa Malta na kipa wao, Andrew Hogg 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ITALIA YASHINDA 1-0 KUFUZU EURO, ILA CROATIA WAMEFANYA BALAA...WAMEMTANDIKA MTU 6-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top