Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MDAU maarufu wa soka nchini, Dk. Philemon Ntahilaja amesema kwamba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limemlea kwa muda mrefu Wakili Dk Damas Ndumbaro akivunja sheria za mchezo huo nchini.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana, Ntahilaja, maarufu Dk Philemon amesema kwamba Ndumbaro baada ya kuwa wakala wa wachezaji anayetambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) hakutakiwa kujihusisha na klabu au chama cha soka chochote.
Ntahilaja, kiongozi wa zamani wa Yanga SC chini ya Tarimba Abbas, amesema FIFA inakataza mawakala kujihusisha na klabu ili kuepuka mgongano wa kamaslahi.
“Ifike pahala tukubaliane kwamba, mtu mmoja asitake kula keki yote peke yake. Leo match agent (wakala wa mechi), kesho players agent (wakala wa wachezaji), kesho kutwa kiongozi wa Kamati ya TFF na klabu,” amesema Dk Ntahilaja na kuongeza;
“Sheria za FIFA zinakataa mgongano huo wa kimasilahi kwa makusudi muhimu, kwa hivyo TFF imemlea sana huyu mtu, matokeo yake ndiyo analeta vurugu zote hizi,”amesema Mjumbe huyo wa Kamati mbalimbali za TFF tangu enzi za Alhaj Muhiddin Ahmed Ndolanga, rais wa shirikisho hilo.
Kamati ya Nidhamu ya TFF, jana imemfungia kwa miaka saba, Dk Damas Ndumbaro kujihusisha na masuala ya soka ndani na nje ya nchi.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu, Jerome Msemwa aliwaambia Waandishi wa Habari kwamba, Ndumbaro amefungiwa baada ya kukutwa na makosa mawili.
Alisema baada ya kikao chao cha siku mbili mwishoni mwa wiki, wamemfungia Ndumbaro mwaka mmoja kwa kosa la kwanza kutoa taarifa zisizo sahihi kiasi cha kupotosha mamuzi ya TFF kinyume cha kanuni nambari 41 kifungu kidogo cha sita cha kanuni za Ligi toleo la mwaka 2014.
Aidha, Wakili huyo pia amefungiwa miaka saba kwa kosa la pili, ambalo ni kushawishi au kupotosha na kuzuia maamuzi ya TFF kupitia bodi ya Ligi kinyume cha kanuni ya nne kifungu kidogo cha 16 toleo la mwaka 2014.
Hata hivyo, Msemwa amesema pamoja na kwamba adhabu ya jumla inakuwa miaka nane, lakini Ndumbaro atatumikia adhabu hiyo kwa miaka saba, kwa kuwa mwaka mmoja upo ndani ya miaka saba.
Akifafanua, Msemwa alisema kwamba Wakili Ndumbaro akiwa mwanafamilia wa TFF kwa vyeo vyake vya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya klabu ya Simba na Mjumbe wa Bodi ya Ligi, alikubali kuziwakilisha klabu dhidi ya TFF.
Alisema kufanya hivyo ni makosa kwa sababu yeye yumo ndani ya TFF na maana yake anajua siri za shirikisho, kwa hivyo alitakiwa kukataa.
Alisema pia, Ndumbaro aliupotosha umma kwa kusema klabu 12 zilimuomba kuziwakilisha kupinga makato ya asilimia tano za fedha za udhamini wa Ligi Kuu, wakati klabu nyingine zilikana kuhusika na mpango huo, Coastal Union na Stand United.
Msemwa alisema kwamba pia Kamati yake ilitilia shaka kama klabu ya Yanga ilikubali kuwakilishwa na Ndumbaro kwa sababu anatoka kwa mahasimu wao, Simba SC.
Wakili Ndumbaro aliitwa kwenye kikao cha Kamati hiyo ya Nidhamu, lakini akasema hataweza kuhudhuria kwa sababu anasafiri nje ya nchi- lakini hiyo haikuzuia Kamati hiyo kukutana na kufikia maamuzi hayo.
Kupitia kampuni yake ya Uwakili ya Meleta & Ndumbaro, Ndumbaro alisema ametumwa na klabu kupinga juu ya mpango wa TFF kukata asilimia tano za fedha za udhamini za Ligi Kuu.
Ndumbaro ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Ligi wa kuteuliwa- aliwaandikia barua TFF kupitia kampuni yake ya uwakili, Meleta & Ndumbaro kuwazuia kukata asilimia tano ya fedha za udhamini wa Ligi Kuu kwa sababu ni kinyume cha mikataba ya Vodacom, wadhamini na akatishia kuitisha mkutano Mkuu wa kumng’oa Malinzi madarakani.
Pamoja na vyeo vyote alivyokuwa kuwa navyo, Ndumbaro ni wakala wa wachezaji anayetambuliwa na FIFA, ambaye moja ya matunda yake ni mchezaji Thomas Emmanuel Ulimwengu anayechezea TP Mazembe ya DRC kwa sasa.
Lakini Ndumbaro Soccer Agent, imepeleka vijana hadi Ulaya, ikiwemo Sweden na Ujerumani ambako karibu kila mwaka hupeleka wachezaji chipukizi.

![]() |
Dk Philemon Ntahilaja |

Rungu la TFF limemshukia Dk Ndumbaro kulia |

0 comments:
Post a Comment