• HABARI MPYA

    Saturday, October 18, 2014

    TANGU 5-0, SIMBA HAIJAFUNGA TENA YANGA SC LIGI KUU

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    SIMBA SC leo itawania kuifunga Yanga SC kwa mara ya kwanza katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara tangu Mei 6, mwaka 2012 walipowafunga watani wao hao wa jadi mabao 5-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam,
    Baada ya kipigo hicho cha kushitua katika mechi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu, Yanga SC imejiimarisha na kutokubali kufungwa na watani wao hao katika mechi zilizofuata za Ligi Kuu hadi sasa.
    Tangu ushindi huo uliotokana na mabao ya Emmanuel Okwi mawili dakika ya pili na 62, Felix Sunzu kwa penalti dakika ya 56, Juma Kaseja kwa penalti pia dakika ya 67 na Patrick Mafisango (marehemu) kwa penalti dakika ya 72, timu hizo zimekutana mara nne zaidi katika Ligi Kuu.

    5-0; Simba SC haijaweza tena kuifunga Yanga SC tangu iichape 5-0 Mei 6, 2012 katika Ligi Kuu ya Bara

    SIMBA NA YANGA TANGU 5-0 ZA MEI 6, 2012 TAIFA

    MEI 6, 2012
    Simba 5-0 Yanga SC
    WAFUNGAJI: 
    Emmanuel Okwi (dk 2 na 62), Felix Sunzu (penalti 56), Juma Kaseja (penalti dk 67) na Patrick Mafisango (penalti dk 72)
    (Ligi Kuu)
    OKTOBA 3, 2013
    Simba 1-1 Yanga SC
    Simba SC: Amri Kiemba dk3
    Yanga SC: Said Bahanuzi dk65
    (Ligi Kuu)
    MEI 18, 2013
    Yanga 2-0 Simba SC
    WAFUNGAJI: Didier Kavumbangu dk 5 na Hamisi Kiiza dk 62.
    OKTOBA 20, 2013
    Yanga SC 3-3 Simba SC
    Yanga SC: Mrisho Ngassa dk15, Hamisi Kiiza dk36 na 45
    Simba SC: Betram Mombeki dk54, Joseph Owino dk58 na Gilbert Kaze dk85.
    APRILI 19, 2014
    Yanga SC 1-1 Simba
    Simba SC: Haroun Chanongo dk76
    Yanga SC: Simon Msuva dk86
    Oktoba 3, 2013 zilitoka sare ya 1-1, Amri Kiemba akitangulia kuifungia Simba SC dakika ya tatu, kabla ya Said Bahanuzi kuisawazishia Yanga SC kwa penalti dakika ya 65.
    Mei 18, mwaka 2013,  Yanga ilishinda mabao 2-0, yaliyotiwa kimiani na Didier Kavumbangu dakika ya tano na Hamisi Kiiza dakika ya 62.
    Oktoba 20, mwaka 2013 timu hizo zilitoka sare ya 3-3, Yanga wakitangulia kufunga kipindi cha kwanza mabao ya Mrisho Ngassa dakika ya 15 na Hamisi Kiiza dakika ya 36 na 45, kabla ya Simba SC kusawazisha kipindi cha pili kupitia kwa Betram Mombeki dakika ya 54, Joseph Owino dakika ya 58 na Gilbert Kaze dakika ya 85.
    Mara ya mwisho zilipokutana Aprili 19, mwaka 2014 timu hizo zilitoka sare ya 1-1, Haroun Chanongo akitangulia kuifungia Simba SC dakika ya 76 kabla ya Simon Msuva kuisawazishia Yanga SC dakika ya 86.
    Hali hiyo ni tofauti sana na Simba SC ilipotoka kuifunga Yanga SC mabao 6-0 Julai 19, mwaka 1977, kwani iliendeleza ubabe wake kwa miaka mitatu zaidi. 
    Baada ya ushindi huo uliotokana na mabao ya 
    Abdallah Kibadeni dakika ya 10, 42 na 89, Jumanne Hassan 'Masimenti' dakika ya 60 na 73 na Selemani Sanga aliyejifunga dakika ya 20, timu, Yanga SC ilikuja kufuta uteja katika mechi ya tatu.
    Oktoba 7, mwaka 1979 Simba iliichapa 3-1, mabao yake yakifungwa na Nico Njohole dakika ya tatu, Mohammed Bakari 'Tall' dakika ya 38 na Abbas Dilunga dakika ya72, baada ya wapinzani wao kutangulia kwa bao la Rashidi Hanzuruni dakika ya nne.
    Oktoba 4, mwaka 1980 Simba iliichapa Yanga 3-0, mabao ya Abdallah Mwinyimkuu dakika ya 29, Thuwein Ally dakika ya 82 na Nico Njohole dakika ya 83.
    Yanga SC ilikuja kujikomboa kwenye makucha ya Simba Septemba 5, mwaka 1981 kwa ushindi wa 1-0, bao pekee la marehemu Juma Hassan Mkambi ‘Jenerali’ dakika ya 42.
    Sasa leo, Wekundu wa Msimbazi watawania kuifungia tena Yanga SC tangu Mei 6, mwaka 2012.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TANGU 5-0, SIMBA HAIJAFUNGA TENA YANGA SC LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top