• HABARI MPYA

    Saturday, October 18, 2014

    MAXIMO NA PHIRI KABLA NA BAADA YA LEO SIMBA NA YANGA...

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    FANYA yote, shinda mataji uwezavyo, lakini ukiwa kocha wa Simba au Yanga, kama hutaweza kushinda mechi ya watani, kibarua chako kipo shakani.
    Simba na Yanga SC zinakutana leo katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, zikiongozwa na makocha wawili tofauti.
    Katika benchi la Simba SC kuna Mzambia Patrick Phiri na kwenye benchi la Yanga SC, kuna Mbrazil, Marcio Maximo.
    Nani atacheka? Kocha Marcio Maximo wa Yanga SC akizungumza na Patrick Phiri wa Simba SC baada ya kukutana Zanzibar Agosti mwaka huu

    REKODI YA MARCIO MAXIMO YANGA SC

    Yanga SC 1-0 Chipukizi (Kirafiki Pemba)
    Yanga 2-0 Shangani (Kirafiki Zanzibar)
    Yanga SC 2-0 KMKM (Kirafiki Zanzibar)
    Yanga SC 1-0 Thika United (Kirafiki Taifa)
    Yanga SC 3-0 Azam FC (Ngao ya Jamii)
    Yanga SC 0-2 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu)
    Yanga SC 2-1 Prisons (Ligi Kuu)
    Yanga SC 2-1 JKT Ruvu (Ligi Kuu)
    Phiri ameajiriwa tena Simba SC msimu huu kwa mara ya nne baada ya awali kufundisha timu hiyo kwa awamu tatu tofauti- tena kwa mafanikio wakati Maximo aliyewahi kufundisha timu ya taifa, Taifa Stars anafanya kazi kwa mara ya kwanza msimu huu Yanga SC.
    Lakini walimu hawa wanafahamiana na wanaheshimiana, kwani wakati Phiri anafundisha Simba SC awali, Maximo alikuwa kocha wa Taifa Stars.
    Tangu amerudishwa Agosti mwaka huu kurithi mikoba ya Mcroatia, Zdravko Logarusi, Phiri amekwishaiongoza Simba SC katika mechi 12, kati ya hizo akishinda nne, kufungwa tatu na sare tano.
    Tangu ameanza kazi Yanga SC Julai mwaka huu kuchukua nafasi ya Mholanzi, Hans va der Pluijm, Maximo amekwishaiongoza Yanga SC katika mechi nane, akishinda saba na kufungwa moja.
    Wote wana jukumu la kuzipa timu zao ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu- lakini ili ndoto za kuendelea kupigania ufamle wa soka nchini ziwe hai, watahitaji matokeo mazuri katika mchezo wa leo.
    Kwa tamaduni za klabu hizo, haitakuwa ajabu yeyote atakayepoteza mechi ya leo akatupiwa virago. 

    REKODI YA PATRICK PHIRI TANGU ARUDI SIMBA SC

    Simba SC 2-1 Kilimani City (Kirafiki Zanzibar)
    Simba SC 2-0 Mafunzo (Kirafiki Zanzibar)
    Simba SC 5-0 KMKM (Kirarfiki, Zanziabr)
    Simba SC 3-0 Gor Mahia (Kirafiki, Dar es Salaam)
    Simba SC 0-1 URA (Kirafiki, Dar es Salaam)
    Simba SC 0-0 Ndanda (Kirafiki Mtwara)
    Simba SC 2-2 Coastal Union (Ligi Kuu)
    Simba SC 1-1 Polisi Moro (Ligi Kuu)
    Simba SC 1-1 Stand United (Ligi Kuu)
    Simba SC 0-0 Orlando Pirates (Kirafiki, Afrika Kusini) 
    Simba SC 2-4 Bidvest Wits (Kirafiki, Afrika Kusini) 
    Simba SC 0-2 Jomo Cosmos (Kirafiki, Afrika Kusini) 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAXIMO NA PHIRI KABLA NA BAADA YA LEO SIMBA NA YANGA... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top