Na Mahmoud Zubeiry, MBEYA
MCHEZO wa mwisho kuzikutanisha timu hizo Uwanja wa Sokoine, Mbeya ulitawaliwa na vurugu baada ya Mbeya City kutaka kugombea bao la ushindi la Azam FC lililofungwa na Nahodha John Bocco ‘Adebayor’ Aprili 13, mwaka huu.
Katika mchezo huo wa pili kuelekea mwisho wa msimu uliopita wa Ligi Kuu, Azam walitangulia kupata bao dakika ya 43 mfungaji, Gaucence Mwaikimba, kabla ya Mbeya City kusawazisha dakika ya 70 kupitia kwa Mwagane Yeya.
Awali ya hapo, katika mchezo wa kwanza timu hizo zilitoka sare ya 3-3 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Azam FC ipo Mbeya tangu Jumatano ikifanya mazoezi ili kuzoea hali ya hewa kabla ya mechi na Mbeya City wameendelea kujifua nyumbani kwao kama kawaida.
Mchezo huo umeteka hisia za mashabiki wa soka Mbeya, wengi wakitamba watalipa kisasi kwa Azam FC huku wakiuponda ushindi wao wa Aprili 13 ulikua wa ‘kubebwa’.
Upande wa Azam FC, hakuna majigambo zaidi ya maandalizi ya kimyakimya kwa ajili ya kuchukua pointi tatu muhimu.
Kila timu imeboresha kikosi chake kutoka cha msimu uliopita, safu ya ushambuliaji ya Azam FC ikiongezea nguvu na mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Mrundi Didier Kavumbangu na Mbeya City wakiwa na mshambuliaji wa zamani wa Kagera Sugar, Themi Felix.
Timu zote hadi sasa hazijapoteza mechi katika Ligi Kuu, lakini Mbeya City inayomilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya imetoa sare mbili na kushinda moja, wakati Azam FC inayomilikiwa na mfanyabiashara Alhaj Sheikh Said Salim Bakhresa na familia yake imeshinda mbili na sare moja.
Mbeya City, inayodhaminiwa na kampuni ya Bin Slum Tyres Limited kupitia betri za RB ikishinda leo itaifikia Azam FC inayodhaminiwa na benki ya NMB kwa pointi na hilo pia linachangia uhondo wa mchezo wa leo. Je, nani ataibuka mbabe Sokone leo? Bila shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona.

![]() |
Wachezaji wa Mbeya City wakimzonga refa baada ya Azam FC kupata bao la ushindi Aprili 13, mwaka huu |

0 comments:
Post a Comment