Na Princess Asia, JOHANNESBURG
SIMBA SC imetoa sare ya bila kufungana na wenyeji Orlando Pirates katika mchezo wa kirafiki asubuhi ya leo Uwanja wa Rand mjini Johannesburg, Afrika Kusini.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe alikuwepo kwenye mchezo huo na baada ya mechi akasema; “Nimefurahishwa na kiwango cha timu japokuwa tulikosa baadhi ya wachezaji wetu walio timu za taifa za Tanzania na Uganda,”.
Mchezo huo ulikuwa sehemu ya maandalizi yake ya mechi dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga SC, Oktoba 18, mwaka huu Dar e Salaam, mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Katika mchezo huo, Simba SC iliwakosa wachezaji wake walio timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars mabeki Miraji Adam na Joram Mgeveke na viungo Jonas Mkude, Amri Kiemba, Said Ndemla na Haruna Chanongo ambao wote watakwenda Afrika Kusini Jumatatu.
Simba SC pia ilimkosa mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi aliyekwenda kujiunga na The Cranes. Okwi hatakwenda kabisa Afrika Kusini, kwa sababu timu yake hiyo ya taifa itakuwa na mechi ya kufuzu AFCON katikati ya wiki dhidi ya Togo mjini Lome.
Simba SC imefikia katika hoteli ya Eden Vale Petra na inafanya mazoezi kwenye viwanja wa Eden Vale mjini Johannesburg.
Simba SC itaendelea kuwa huko ikifanya mazoezi ya nguvu hadi Oktoba 17 itakaporejea Dar es Salaam, ikiwa ni siku moja kabla ya mechi na watani. Kuna mpango wa mechi moja zaidi ya kirafiki.
Baada ya sare tatu mfululizo katika mechi zake tatu za awali, 2-2 na Coastal Union, 1-1 mara mbili na Polisi Moro na Stand United, Simba SC imepania kushinda mechi ya kwanza Oktoba 18.

![]() |
Hatari kwenye lango la Simba SC; Wachezaji wa Orlando Pirates wakishambulia leo |
Katika mchezo huo, Simba SC iliwakosa wachezaji wake walio timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars mabeki Miraji Adam na Joram Mgeveke na viungo Jonas Mkude, Amri Kiemba, Said Ndemla na Haruna Chanongo ambao wote watakwenda Afrika Kusini Jumatatu.
Simba SC pia ilimkosa mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi aliyekwenda kujiunga na The Cranes. Okwi hatakwenda kabisa Afrika Kusini, kwa sababu timu yake hiyo ya taifa itakuwa na mechi ya kufuzu AFCON katikati ya wiki dhidi ya Togo mjini Lome.
Simba SC imefikia katika hoteli ya Eden Vale Petra na inafanya mazoezi kwenye viwanja wa Eden Vale mjini Johannesburg.
![]() |
Wachezaji wa Simba SC na Orlando Pirates katika picha ya pamoja kabla ya mechi |
![]() |
Simba SC wakitoka uwanjani baada ya mechi |
Simba SC itaendelea kuwa huko ikifanya mazoezi ya nguvu hadi Oktoba 17 itakaporejea Dar es Salaam, ikiwa ni siku moja kabla ya mechi na watani. Kuna mpango wa mechi moja zaidi ya kirafiki.
Baada ya sare tatu mfululizo katika mechi zake tatu za awali, 2-2 na Coastal Union, 1-1 mara mbili na Polisi Moro na Stand United, Simba SC imepania kushinda mechi ya kwanza Oktoba 18.
0 comments:
Post a Comment