• HABARI MPYA

    Saturday, October 11, 2014

    RANGERS YAIKALISHA LIPULI KARUME, JULIO NA MWADUI YAKE WALA KICHAPO KWA TOTO AFRICAN LIGI DARAJA LA KWANZA

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    KLABU ya Friends Rangers ya Manzese, Dar es Salaam leo imeanza vyema msimu mpya wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara baada ya kuichapa mabao 2-1 Lipuli ya Iringa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam. 
    Lipuli iliyowahi kutamba katika Ligi Kuu miaka ya 1990, ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 30 kupitia kwa Abdallah Mussa, kabla ya Yussuf Mkinda kuiswazishia Rangers dakika ya 34 kwa penalti kufuatia mchezaji wa Lipuli, kuunawa mpira kwenye eneo la hatari. 
    Julio leo ameanza vibaya Daraja la Kwanza baada ya kufungwa na Toto

    Rangers ilipata bao lake la ushindi kupitia kwa mshambuliaji wa zamani wa Simba SC na Mtibwa Sugar, Yusuph Mgwao ‘Shemeji’, dakika za lala salama. 
    Katika mchezo mwingine wa Ligi hiyo, Mwadui FC inayofundishwa na kocha maarufu, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ imelala 1-0 mbele ya Toto Africa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza bao pekee la Andusi Issa dakika ya 75. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RANGERS YAIKALISHA LIPULI KARUME, JULIO NA MWADUI YAKE WALA KICHAPO KWA TOTO AFRICAN LIGI DARAJA LA KWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top