• HABARI MPYA

    Tuesday, October 14, 2014

    GARETH BALE AING’ARISHA WALES KUFUZU EURO, ISRAEL YAUA 4-1 AKINA EDEN DZEKO WASHIKWA

    NYOTA wa Real Madrid, Gareth Bale ameiongoza timu yake ya taifa, Wales kuilaza 2-1 Cyprus katika mchezo wa Kundi B kufuzu Euro 2016. 
    David Cotterill alitokea kwenye benchi kuchukua nafasi ya nafasi ya Simon Church dakika ya sita na kuifungia bao la kuongoza Wales la kwanza dakika ya 13.
    Hal Robson-Kanu akaifungia bao la pili Wales dakika ya 23 baada ya kazi nzuri ya Bale- kabla ya Vincent Laban kuipatia bao la kufutia machozi Cyprus dakika ya 36. 
    Andy King alilimwa kadi nyekundu ya moja kwa moja, baada ya kumchezea rafu Nahodha wa Cyprus, Constantinos Makrides dakika ya 48. 
    Gareth Bale akipasua katikati ya mabeki wa Cyprus jana

    Wales sasa ina pointi saba baada ya kushinda mechi mbili na sare moja.
    Katika mechi nyingine za kundi hilo, Bosnia-Herzegovina ikiwa nyumbani, imetoka sare ya 1-1 na Ubelgiji bao la wenyeji likifungwa na Eden Dzeko dakika ya 28, kabla ya wageni kusawazisha kupitia kwa Raja Nainggolan dakika ya 51.
    Israel licha ya kuwa ugenini imeifunga Andorra 4-1, mabao yake yakifungwa na Omer Damar matatu na Tommer Hemed wakati la kufutia machozi la wapinzani wao lilifungwa na Ildefons Lima kwa penalti.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GARETH BALE AING’ARISHA WALES KUFUZU EURO, ISRAEL YAUA 4-1 AKINA EDEN DZEKO WASHIKWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top