• HABARI MPYA

    Friday, October 17, 2014

    DEWJI: SIMBA SUBIRINI DAKIKA 90, ACHENI KUWAHOFIA YANGA

    Na Samira Said, DAR ES SALAAM
    ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Simba, Kassim Dewji, amesema kuwa mashabiki wa timu hiyo wanatakiwa kuwa watulivu na kusubiri dakika 90 za mchezo huo.
    Yanga inatarajiwa kuikaribisha Simba katika mechi ya mzunguko wa kwanza ya Ligi Kuu ya Soka Tanzania itakayofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
    Kassim ameiambia BIN ZUBEIRY leo kuwa kikosi cha Simba kiko imara na kinaamini kitapata matokeo mazuri.
    Kassim Dewji kushoto amewataka wana Simba watulie kusubiri dakika 90

    Kiongozi huyo maarufu kwa jina la KD amesema kwamba mechi hiyo kwake inaweza kumfanya akachukua maamuzi tofauti na wadau wa soka wanavyotarajia hasa wale wa Simba.
    "Nimeshasema kila ninapoulizwa kuhusiana na mechi hii...kwa kweli tumejipanga na lolote linaweza kutokea kwa sababu ushindani ni mkubwa...Simba wasiwe na tamaa, wawe watulivu ," ameongeza KD.
    Kassim ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba wa kuteuliwa na Rais wa klabu hiyo, Evans Aveva.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DEWJI: SIMBA SUBIRINI DAKIKA 90, ACHENI KUWAHOFIA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top