• HABARI MPYA

    Saturday, October 11, 2014

    BLATTER AKATAA SHERIA YA MABAO YA UGENINI, ASEMA IMEPITWA NA WAKATI NA HAITENDI HAKI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    RAIS wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Sepp Blatter jana amesema kwamba umefika wakati sheria ya mabao ya ugenini kuipa timu ushindi kufuatia sare ya mechi mbili, ifikie tamati.
    Blatter amesema sheria hiyo inazibeba timu ambazo zinacheza ugenini kwenye mechi za marudiano, kwa sababu muda wa nyongeza unaweza kutoa fursa ya ziada kusaka mabao zaidi.
    “Ni wakati wa kuufikiria upya mfumo huu," amesema Blatter katika kolamu ya toleo la  FIFA wiki hii. Sheria ya mabao ya ugenini inatumika kwenye mechi za mtoano na michuano kama Ligi ya Mabingwa, Afrika na Ulaya na ilianzishwa mwaka 1965.
    Blatter kushoto na Rais wa TFF, Jamal Malinzi

    Baada ya timu mbili kutoka sare kwenye mechi mbili za nyumbani na ugenini, timu ambayo ilifunga mabao zaidi ugenini inasonga mbele.
    “Mawazo haya yamepitwa na wakati, yalikuwa ya enzi ambazo mechi za ugenini zilichukuliwa mzigo, zikihusisha safari ndefu na mazingira tofauti," alisema bosi huyo wa FIFA mwenye umri wa miaka 78.
    Tayari sheria hiyo haitumiki tena katika Nusu Fainali au mechi za kuwania kupanda za Ligi za England.
    Ligi Kuu ya Marekani, na Ligi ya Mabingwa wa Amerika (CONCACAF) wao wanahesabu mabao yaliyofungwa ndani ya dakika 90 tu za kawaida.
    “Soka imepiga hatua tangu miaka ya 1960, hivyo sasa lazima watu wahoji kuhusu sheria ya mabao ya ugenini,” amesema Blatter, ambaye hakushauri njia mbadala.
    TP Mazembe ya DRC mwaka huu imeonja machungu ya sheria ya mabao ya ugenini baada ya kutolewa na ES Setif ya Algeria katika Nusu Fainali ya Ligi Mabingwa Afrika licha ya sare ya jumla ya 4-4.
    Mazembe yenye washambuliaji wawili Watanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu ilifungwa 2-1 katika mchezo wa kwanza Algeria kabla ya kushinda 3-2 katika mchezo wa marudiano Lubumbashi. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BLATTER AKATAA SHERIA YA MABAO YA UGENINI, ASEMA IMEPITWA NA WAKATI NA HAITENDI HAKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top