Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
KOCHA wa Mtibwa Sugar, Mecky Mexime amesema kwamba mchezo wa leo dhidi ya Polisi Uwanja wa Jamhuri, Morogoro utakuwa mgumu, lakini watapigana kushinda ili kujiimarisha kileleni.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY wiki hii, Mexime alisema kwamba timu yao imekuwa katika maandalizi mazuri tangu mchezo wao wa mwisho wakishinda dhidi ya Mgambo JKT Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.
Nahodha huyo wa zamani wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, amesema kwamba wanaiheshimu Polisi ni timu nzuri na ina mwalimu mzuri (Mohamed Adolph Rishard) na wachezaji wazuri pia.
“Lengo letu ni pointi tatu, tutaingia Uwanja wa Jamhuri kupigania pointi tatu. Hicho ndicho nachoweza kukuambia,”amesema Mexime.
Mtibwa Sugar itaingia Uwanja wa Jamhuri leo ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa mabao 2-0 ilipocheza mara ya mwisho hapo katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu dhidi ya Yangs SC ya Dar es Salaam Septemba 20, mwaka huu.
Kwa sasa, Mtibwa ndio wapo kileleni mwa Ligi kwa pointi zao tisa, wakifuatiwa na mabingwa watetezi, Azam FC wenye pointi saba ma Yanga SC pointi sita.

![]() |
Mecky Mexime kulia akiwa na kocha wa Yanga SC, Marcio Maximo |
“Lengo letu ni pointi tatu, tutaingia Uwanja wa Jamhuri kupigania pointi tatu. Hicho ndicho nachoweza kukuambia,”amesema Mexime.
Mtibwa Sugar itaingia Uwanja wa Jamhuri leo ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa mabao 2-0 ilipocheza mara ya mwisho hapo katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu dhidi ya Yangs SC ya Dar es Salaam Septemba 20, mwaka huu.
Kwa sasa, Mtibwa ndio wapo kileleni mwa Ligi kwa pointi zao tisa, wakifuatiwa na mabingwa watetezi, Azam FC wenye pointi saba ma Yanga SC pointi sita.
0 comments:
Post a Comment