KLABU ya Manchester City inaaamini haijavunja sheria ya UEFA ya matumizi fedha kiungwana kwa kumchukua kwa mkopo Frank Lampard.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 36 ameesaini mkataba wa miaka miwili na New York City ya Marekani— moja ya klabu dada za Manchester City.
Lakini timu hiyo ya Marekani livi yao itaanza Machi mwakani, hivyo Lampard atarejea kucheza Ligi Kuu England hadi January.
Kujiamini: Man City haimanini kama imevunja sheri a za matumizi ya fedha kiungwana kwa kumchukua kwa mkopo Frank Lampard
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ameelezea wasiwasi wake juu ya usajili wa Lampard kwa mkopo ni wa ujanja ujanja baada ya FFP kuzuia klabu kutumia fedha kuliko zinazvyoingiza kwenye mpira.
City ilikwama kwenye sheria ya UEFA ya FFP msimu uliopita na inatakiwa kuingiza wachezaji wazawa wanne katika usajili wake wa kikosi cha wachezaji 21 wa kucheza Ligi ya Mabingwa.
Sheria za UEFA zinasema kuhusu usajili wa mkopo Lampard, unaangukia kwenye mtego wa FFP kwa kuwa City sasa ndio watamlipa mshahara mchezaji huyo. Pamoja na hayo, Manchester City, New York City, Melbourne City zote zinamilikiwa na kampuni ya City Football Group — ambao pia wan a hiss Yokohama Marinos.
Zengwe: Arsene Wenger amesema usajili wa Lampard kwenda kwa mkopo Man City umekouka sheria ya UEFA ya FFP
0 comments:
Post a Comment