MSHAMBULIAJI Luis Suarez ameelezea furaha yake ya kuruhusiwa kufanya mazoezi baada ya kujiunga na wachezaji wenzake wa Barcelona kwa mara ya kwanza leo.
Nyota huyo wa Uruguay alilazimika kufanya mazoezi peek yake akisubiri majibu ya rufaa yake Mahakama ya Usuluhishi (CAS) juu ya adhabu ya kutojihusisha na soka kwa miezi mine baada ya kumng'ata Giorgini Chiellini wa Italia katika Kombe la Dunia.
CAS imepunguzia adhabu mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool na sasa hataruhusiwa kucheza mechi za mashindano tu, lakini za kirafiki za klabu na timu ya taifa atacheza.
Mkali huyo wa mabao mwenye umri wa miaka 27 atamaliza adhabu yake Oktoba na kuanza rasmi kucheza La Liga na Barca.
Suarez alikuwa mwenye furaha leo akifanya mazoezi na Barcelona kwa mara ya kwanza tangu asajiliwe
Luis Suarez akijifua na wachezaji wenzake wa Barcelona, akiwemo Nahodha Xavi
Barcelona wanaendelea na maandalizi ya msimu
Luis Suarez akionyesha nembo ya Barcelona kwa furaha baada ya kupunguziwa adhabu na CAS
"Nina furaha sana kuwa tayari kujisikia kama mchezaji tena na kuwa na wachezaji wenzangu wa timu. Nilipagawa mno kuanza mazoezi,".
"Nashukuru sana kwa tote ambayo klabu imenifanyia kwa wiki chache zilizopita. Wamenitendea wema mno na ninashukuru sasa kuwa tayari kuanza changamoto hii kubwa ya kuichezea Barca,".
"Hayakuwa mazingira huru kabisa. Ni malipo ya makosa niliyoyafanya na ninaomba radhi, lakini natakiwa kuyaacha nyuma yangu yote sasa," amesema Suarez.
0 comments:
Post a Comment