• HABARI MPYA

    Sunday, August 17, 2014

    RWANDA YAONDOLEWA MAKUNDI AFCON BAADA YA KUFOJI MCHEZAJI

    Na Mahmoud Zubeiry, KIGALI
    KAMATI ya Maandalizi ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) imeiondoa Rwanda kwenye mbio za kuwania tiketi ya michuano hiyo mwakani Morocco.
    Taarifa ya CAF iliyotumwa BIN ZUBEIRY leo imesema kwamba uamuzi huo unafuatia malalamiko ya Shirikisho la Soka la Kongo (FECOFOOT) wakati wa mechi ya kwanza ya kufuzu dhidi ya Rwanda Julai 20, mwaka 2014 Pointe-Noire.
    Malalamiko ya Kongo yalikuwa kuhusu mchezaji Birori Dady aliyeichezea Rwanda, na akaichezea AS Vita ya Kinshasa, akiwa na pasioti ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa jina la Etekiama Agiti Tady, zikiwa na umri tofauti.
    Mchezaji aliyewaponza Rwanda
    Baada ya uchunguzi wa CAF na vielelezo vilivyowasilishwa na Mashirikisho ya Soka Rwanda, Kongo na DRC, na maelezo ya mchezaji huyo aliyotoa Agosti 11 mwaka 2014 makao makuu ya CAF mjini Cairo, imethibitika watu hao wawili ni mtu huyo huyo mmoja.
    Wakati Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA) limeshiilia msimamo wake wa mchezaji huyo ni Dady Birori, uchunguzi umegundua alipewa jina la Etekiama Agiti Tady na FERWAFA ili achezee timu ya taifa ya Rwanda.
    Kutokana na makos a yaliyogundulika, Kamati ya Maandalizi ya AFCON kwa mujibu wa kanuni ya 41 mashindano hayo ibara ya 82 na 83.1 ya kanuni za adhabu, hatua zifuatazo zimechukuliwa:

    1. Mchezaji Etekiama Agiti Tady au Birori Dady anasimamishwa mara moja kuchezea klabu na timu ya taifa hadi hapo maamuzi zaidi yatakapotolewa.

    2. Rwanda inapoteza mchezo namba  37 dhidi ya Kongo, na mara moja inaondolewa kwenye michuano.

    3. Kongo inaignia kwenye hatua ya Kundi A kuwania tiketi ya AFCON ya Morocco mwaka 2015 ikichukua nafasi ya Rwanda
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RWANDA YAONDOLEWA MAKUNDI AFCON BAADA YA KUFOJI MCHEZAJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top