// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MALINZI AHANI MSIBA WA MAKAMU WA RAIS FIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MALINZI AHANI MSIBA WA MAKAMU WA RAIS FIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, August 05, 2014

    MALINZI AHANI MSIBA WA MAKAMU WA RAIS FIFA

    Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
    RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Shrikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Sepp Blatter kutokana na kifo cha makamu wake mwandamizi Julio Grondora (pichani chini).
    Amesema yeye binafsi na jamii ya mpira wa miguu Tanzania kwa ujumla wanaomboleza msiba wa Grondora ambaye pia alikuwa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Argentina (AFA).

    Ameongeza kuwa Grondora alikuwa mtumishi mwandamizi wa mpira wa miguu, kwani alijitoa katika kuutumikia mpira wa miguu, na mchango wake katika maendeleo ya mchezo huo utaendelea kukumbukwa wakati wote.
    Rais Malinzi amesema familia ya mpira wa miguu nchini Argentina imepata pigo, na ametoa pole kwa familia ya marehemu, AFA na familia nzima ya FIFA na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito. Bwana ametoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe. Amina.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MALINZI AHANI MSIBA WA MAKAMU WA RAIS FIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top