Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
KIUNGO wa Simba SC, Jonas Mkude atakosa mechi kadhaa za mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya goti.
Mkude aliumia akiichezea timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars mwezi uliopita nchini Botswana na baada ya vipimo mjini Dar es Salaam ikagundulika maumivu yake ni makubwa.
Baada ya kupatiwa matibabu, Mkude amesema; “Nimeambiwa natakiwa nipumzike wiki sita, na sasa nipo katika wiki ya pili,”alisema Mkude akizungumza na BIN ZUBEIRY jana Dar es Salaam.
“Kwa kweli nahitaji kutulia nipone kabisa ili nirudi uwanjani nikiwa fiti kabisa, sitaki kuharakisha ili niwe na matatizo ya kudumu. Nataka nipone vizuri kabisa ndipo nirudi uwanjani kwa nguvu mpya,”ameongeza.
Mkude ataanza mazoezi mepesi mwishoni mwa Septemba mwaka huu kipindi ambachio Ligi Kuu itakuwa inaanza (Septemba 20)- maana yake atatarajiwa kuanza kucheza taratibu mwezi mmoja baadaye.
Kuumia kwa Mkude si pigo kwa klabu yake Simba SC, bali hata Taifa Stars ambayo kwa wakati huu inamkosa pia kiungo mwingine, Frank Domayo ambaye pia ni majeruhi.

![]() |
Pigo Msimbazi; Simba SC itamkosa kwa wiki sita Jonas Mkude |
Baada ya kupatiwa matibabu, Mkude amesema; “Nimeambiwa natakiwa nipumzike wiki sita, na sasa nipo katika wiki ya pili,”alisema Mkude akizungumza na BIN ZUBEIRY jana Dar es Salaam.
“Kwa kweli nahitaji kutulia nipone kabisa ili nirudi uwanjani nikiwa fiti kabisa, sitaki kuharakisha ili niwe na matatizo ya kudumu. Nataka nipone vizuri kabisa ndipo nirudi uwanjani kwa nguvu mpya,”ameongeza.
Mkude ataanza mazoezi mepesi mwishoni mwa Septemba mwaka huu kipindi ambachio Ligi Kuu itakuwa inaanza (Septemba 20)- maana yake atatarajiwa kuanza kucheza taratibu mwezi mmoja baadaye.
![]() |
Jonas Mkude kushoto akiwa mchezaji mwenzake wa Simba SC, Ramadhani Singano 'Messi' |
Kuumia kwa Mkude si pigo kwa klabu yake Simba SC, bali hata Taifa Stars ambayo kwa wakati huu inamkosa pia kiungo mwingine, Frank Domayo ambaye pia ni majeruhi.
0 comments:
Post a Comment