• HABARI MPYA

    Thursday, June 12, 2014

    ROONEY AMFUNGULIA DOMO RONALDO, AMUAMBIA "UNAPENDA UBINFASI, MIMI MJAMAA"

    MSHAMBULIAJI Wayne Rooney amesema mchezaji mwenzake wa zamani wa Manchester United, Cristiano Ronaldo anavutiwa mafanikio binafsi kuelekea Kombe la Dunia, michuano inayoanza usiku wa leo Brazil.
    Rooney amesema Ronaldo ni mtu anayependa mafanikio binafsi.
    Ronaldo alivua jezi yake ya Real Madrid na kwenda kuweka pozi mbele ya kamera baada ya kuifungia timu hiyo bao la nne kwa penalti katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Atletico Madrid, zote za Hispania kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwezi uliopita. 
    Ametulia: Wayne Rooney amesema anapenda mafanikio ya timu kuliko binafsi
    Star man: Cristiano Ronaldo takes a shot in Portugal's 5-1 win over the Republic of Ireland
    Nyota: Cristiano Ronaldo akipiga shut katika ushindi wa Ureno wa 5-1 dhidi ya Jamhuri yaf Ireland juzi kwenye mchezo wa kirafiki

    Rooney, aliyecheza na Ronaldo kuanzia mwaka 2004 hadi 2009, amesema: "Mimi si mchezaji mpenda makuu – kama Cristiano, anataka sana hayo mambo. Nipo kwa ajili ya ushindi wa timu zaidi. Anapenda kuwa na wakati wake. Nimeshinea tuzo ya mchezaji bora wa mwaka, hakuna kitu kizuri kama kushinda taji na United,".
    Wakati huo huo, Rooney anaamini kwamba hakuna cha kuhofia kwa kwa wachezaji wawili wa Juventus, Leonardo Bonucci na Giorgio Chiellini, ambao England itakutana nao katika mchezo wa ufunguzi wa Kombe la Dunia mjini Manaus.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ROONEY AMFUNGULIA DOMO RONALDO, AMUAMBIA "UNAPENDA UBINFASI, MIMI MJAMAA" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top