• HABARI MPYA

  Jumanne, Juni 24, 2014

  TFF YAMPA HONGERA MKWASA KUPATA KAZI UATABUNI

  Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limempongeza Kocha mzawa Charles Boniface Mkwasa kwa kupata ajira ya ukocha msaidizi katika klabu Shoalah nchini Saudi Arabia.
  “Tunatoka mwito kwa makocha wengine kuiga mfano wa Mkwasa, kwani kufundisha mpira wa miguu nje ya Tanzania si tu kunawaongezea ujuzi bali pia kunawapa fursa ya kufanya kazi katika mazingira tofauti,”imesema TFF katika taarifa yake.
  Charles Boniface Mkwasa

  Huko nyuma baadhi ya makocha wa Tanzania kama Mansour Magram, Kinanda Zakaria na Sunday Kayuni waliwahi kufundisha mpira wa miguu nje. Tangu wakati huo hakuna rekodi zinazoonesha kuwa kina makocha wazawa wanaofundisha nje.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TFF YAMPA HONGERA MKWASA KUPATA KAZI UATABUNI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top