• HABARI MPYA

  Jumapili, Juni 29, 2014

  UHOLANZI YATINGA ROBO FAINALI KWA MBINDE, YAICHAPA MEXICO 2-1

  UHOLANZI imeenda Robo Fainali ya Kombe la Dunia baada ya kuifunga Mexico mabao 2-1 ikitoka nyuma kwa 1-0 jioni hii nchini Brazil.
  Shkurani kwake, Klaas-Jan Huntelaar aliyefunga kwa penalti bao la ushindi dakika ya nne ya muda wa nyongeza baada ya kutimu dakika 90 za kawaida, baada ya Arjen Robben kuangushwa kwenye boksi  na Marquez.
  Babu kubwa: Klaas-Jan Huntelaar akishangilia baada ya kufunga bao la ushindi Uholanzi ikienda Roibo Fainali
  Winner: Huntelaar celebrates scoring the dramatic late goal for the Dutch
  Huntelaar akisherehekea bao lake muhimu
  Level: Wesley Sneijder scored in the 88th minute to drag Holland bag into the game
  La kusawazisha: Wesley Sneijder alifunga bao la kusawazisha dakika ya 88 na kuwakata maini Mexico

  Awali ya hapo, Wesley Sneidjer aliifungia bao la kusawazisha Uholanzi dakika ya 88 kufuatia 
  Giovani dos Santos kutangulia kuifungia Mexico dakika ya 48.
  Kikosi cha Uholanzi kilikuwa; Cillessen, Vlaar, De Vrij, Verhaegh/Depay dk56, Kuyt, Wijnaldum, De Jong/Martins Indi dk9, Blind, Sneijder, Robben na Van Persie/Huntelaar dk76.
  Mexico: Ochoa, Aguilar, Rodriguez, Marquez, Moreno/Reyes dk46, Layun, Salcido, Herrera, Guardado, Giovani/Aquino dk61 na Peralta/Hernandez dk75.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: UHOLANZI YATINGA ROBO FAINALI KWA MBINDE, YAICHAPA MEXICO 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top