• HABARI MPYA

  Jumapili, Juni 22, 2014

  FABREGAS ATIMULIWA MAZOEZINI NA DEL BOSQUE HISPANIA

  MCHEZAJI mpya wa Chelsea, Cesc Fabregas amedaiwa kuzinguana na kocha wake wa timu ya taifa ya Hispania, Vicente del Bosque hadi kufukuzwa mazoezini nchini Brazil.
  Hasira zimekuwa za hali ya juu katika kambi ya Hispania baada ya timu hiyo kuvuliwa ubingwa na kutolewa mapema Kombe la Dunia kwa kufungwa na Uholanzi na Chile.
  Del Bosque hakuvtiwana ufanyaji mazoezi wa Fabregas katakana na kutofuata maelekezo yake. 
  Nipishe, nenda nje: Hamkani si shwari katika kambi ya Hispania

  Baada ya kuona kuchoshwa na haki hiyo, Del Bosque akamtaka Fabregas ague bipu na kumkabidhi Xabi Alonso na kuondoka kabisa mazoezini.
  Nyota huyo wa zamani wa Arsenal na Barcelona alichukizwa na jambo hilo, huku wachezaji wenzake wakimzuia kubishana zaidi na Del Bosque.
  Inaaminika Fabregas alikasirishwa na kutolewa kwa Hispania na pia kuingizwa kama mchezaji wa tatu wa kutokea benchi katika kipigo cha 5-1 kutoka kwa Uholanzi, na kutotumika kabisa dhidi ya Chile.
  Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 jumla amecheza dakika 12 tu katika Kombe la Dunia mwaak huu hadi sasa.
  Del Bosque anafahamika kama mtu mwenye huruma sana na mwepesi kusamahe na haitakuwa ajabu Fabregas akianza katika mchezo wa mwisho wa Hispania dhidi ya Australia, kocha huyo akijaribu kutafuta kikosi kipya cha kumtoa mrithi japo kwa ushindi wa mechi moja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: FABREGAS ATIMULIWA MAZOEZINI NA DEL BOSQUE HISPANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top