• HABARI MPYA

  Jumanne, Juni 24, 2014

  HABABUU ATEULIWA KUINOA SERENGETI BOYS

  Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
  KOCHA Hababuu Ali Omar ameteuliwa kukinoa kikosi cha wachezaji 39 cha timu ya Taifa ya Tanzania kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Seregenti Boys) ambacho kimeingia kambini leo (Juni 24 mwaka huu) kujiandaa kwa mechi ya michuano ya Afrika dhidi ya Afrika Kusini (Amajimbos).
  Hababuu ambaye ana uzoefu wa miaka 18 katika timu za vijana na ameita wachezaji 39 katika kikosi cha awali ambacho baada ya wiki moja atakipunguza na kubaki na wachezaji 25 aliaanza kufundisha timu za vijana Zanzibar tangu mwaka 1996.

  Akiwa na vyeti vinane tofauti vya ukocha ikiwemo Leseni B inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), amefundisha mpira katika madaraja tofauti visiwani Zanzibar, na baadaye kuwa kocha msaidizi wa timu za vijana za Tanzania kwa umri chini ya miaka 20 na 12 hadi mwaka 2012.
  Mshauri wa Ufundi wa timu hiyo atakuwa Stewart John Hall. Mechi dhidi ya Afrika Kusini itachezwa Julai 18 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam wakati ile ya marudiano itakuwa wiki mbili baadaye nchini Afrika Kusini.
  Wachezaji wa Serengeti Boys walioko kambini ni Zidi Abdalla (Zanzibar), Salum Hamis (Dar es Salaam), Arafat Stambuli (Dar es Salaam), Sabri Shaaban (Kinondoni), Seif Seleman (Kipingu Academy), Baraka Yusuf (Kipingu Academy), Said Mohamed (Zanzibar), Seif Said (Zanzibar) na Adam Daruwesh (Kipingu Academy).
  Adam Ali (Zanzibar), Shaaban Pandu (Zanzibar), Yahya Adnan (Zanzibar), Omar Ame (Zanzibar), Abdulrasul Bitebo (Dar es Salaam), Juma Ali (Zanzibar), Mussa Shaaban (Zanzibar), Hatibu Yasin (Arusha), Athanas Eminias (Kipingu Academy), Nazir Abdul (Arusha), Badru Haji (Kipingu Academy) na Joseph Daniel (Arusha).
  Paul Malamla (Morogoro), Omar Natalis (Dar es Salaam), Joseph Prosper (Dar es Salaam), Ramadhan Soloka (Arusha), Mohamed Mussa (Morogoro), Kelvin Richard (Mwanza), Mashaka Said (Mwanza), Abdultalib Hamidu (Morogoro), Martin Kigo (Mwanza) na Salim Siasa (Temeke).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HABABUU ATEULIWA KUINOA SERENGETI BOYS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top