• HABARI MPYA

  Jumatatu, Juni 23, 2014

  RONALDO NA URENO WAONYESHWA UWANJA WA NDEGE ULIPO KOMBE LA DUNIA

  URENO imepata pointi ya kwanza katika Kombe la Dunia baada ya sare ya 2-2 na Marekani usiku wa kuamkia leo, lakini bado iko mguu nje kwenye michuano hiyo.
  Ureno sasa itabidi iifunge Ghana katika mchezo wa mwisho na iombe Marekani ifungwe na Ujerumani- ili kufuzu 16 Bora. Ujerumani inaongoza Kundi G kwa wastani wa mabao, ikiwa na pointi zake nne sawa na Marekani, wakati Ghana na Ureno zina pointi moja kila moja. 
  Mabao ya Marekani yalifungwa na Jones dakika ya 65 na Dempsey dakika ya 81, wakati ya Ureno yalifungwa na Nani dakika ya tano na Varela dakika ya tano ya muda wa nyongeza baada ya kutimu dakika 90 za kawaida.
  Kikosi cha Marekani kilikuwa; Howard, Johnson, Cameron, Besler, Beasley, Beckerman, Jones, Bedoya/Yedlin dk72, Bradley, Zusi/Gonzales dk90 na Dempsey.
  Ureno; Beto, Pereira, Costa, Alves, Almeida/Carvalho dk45, Moutinho, Veloso, Meireles/Varela dk68, Ronaldo, Postiga/Eder dk15 na Nani.
  Mguu nje: Cristiano Ronaldo akiwatoka mabeki wa Marekani jana
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RONALDO NA URENO WAONYESHWA UWANJA WA NDEGE ULIPO KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top