• HABARI MPYA

  Ijumaa, Juni 27, 2014

  LUKE SHAW AKAMILISHA MAN UNITED NA KUKABIDHIWA UZI, AHAKIKISHIWA KUMUWEKA BENCHI EVRA

  BEKI wa kimataifa wa England, Luke Shaw amekamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 31.5 kutua Manchester United kwa mkataba wa miaka minne kupiga kazi Old Trafford.
  Mchezaji huyo amekamilisha vizuri vipimo afya katika Uwanja wa mazoezi wa United, Carrington na ameambiwa atakuwa beki wa kushoto chaguo la kwanza la kocha Louis van Gaal.
  Inafahamika amehakikishiwa mamba na beki mkongwe mwenye umri wa miaka 33, Patrice Evra, ambaye atabakia United, anatarajiwa kupunguziwa majukumu klabuni hapo. 
  Mambo safi: Luke Shaw akiwa ameshika jezi ya Man United baada ya kukamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 31.5
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LUKE SHAW AKAMILISHA MAN UNITED NA KUKABIDHIWA UZI, AHAKIKISHIWA KUMUWEKA BENCHI EVRA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top