• HABARI MPYA

  Jumapili, Juni 22, 2014

  UBELGIJI YATINGA 16 BORA KOMBE LA DUNIA, YAWAACHIA KIMBEMBE ALGERIA, KOREA NA URUSI

  Mtokea benchi babu kubwa: Divock Origi kulia akipongezwa na mchezaji mwenzake, Kevin Mirallas baada ya kuifungia Ubelgiji bao pekee la ushindi dhidi ya Urusi katika mchezo wa Kundi H Kombe la Dunia. Ubelgiji inafuzu 16 Bora ya michuano hiyo inayoendelea Brazil kwa kufikisha pointi sita baada ya mechi mbili. Nafasi ya pili ya kufuzu kutoka kundi hilo bado iko wazi kwa timu nyingine zote tatu, Algeria, Jamhuri ya Korea zitakazomenyana baadaye na Urusi. Urusi na Korea zina pointi moja kila moja, wakati Algeria haina pointi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: UBELGIJI YATINGA 16 BORA KOMBE LA DUNIA, YAWAACHIA KIMBEMBE ALGERIA, KOREA NA URUSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top