RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi mwishoni mwa wiki aliiagiza Simba SC ya Dar es Salaam kusitisha kwanza mchakato wa uchaguzi hadi hapo klabu hiyo itakapounda Kamati ya Maadili ambayo itasikiliza masuala ya kimaadili kuelekea uchaguzi huo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu ya TFF, katikati ya Jiji la Dar es Salaam Jumapili mchana, Malinzi alisema kwamba Simba SC inatakiwa kuwa imekwishaunda Kamati ya Maadili hadi kufika Juni 30, mwaka huu.
Malinzi alisema kwamba hatua hiyo imefuatia TFF kupokea malalamiko mengi juu ya ukiukwaji wa maadili kwa baadhi ya wagombea na wanachama wa klabu hiyo.
Malinzi alisema kwamba baada ya kuundwa kwa Kamati hiyo Maadili itasikiliza malalamiko yote ya kimaadili yanayougubika mchakato wa udhaguzi huo, ambao awali ulipangwa kufanyika Juni 29, mwaka huu.
Malinzi alisema kwamba kwa sasa Kamati ya Utendaji ya Simba SC iliyopo madarakani chini ya Mwenyeiiti wake, Alhaj Ismail Aden Rage itaendelea kuiongoza klabu hiyo hadi hapo mchakato wa uchaguzi utakapokamilika.
Siku iliyofuata, Jumatatu- Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC, Wakili Dk Damas Daniel Ndumbaro akasema TFF haina mamlaka kikatiba kusimamisha uchaguzi wa klabu hiyo, na maana yake uchaguzi huo upo kama ulivyopangwa kufanyika Juni 29, mwaka huu.
Na kuhusu Kamati ya Maadili, Ndumbaro alisema kwa kutambua Simba SC haina Kamati ya Maadili, ndiyo maana alizipeleka kesi za kimaadili kwa Kamati ya Maadili ya TFF.
Ndumbaro, akasema kama TFF iliweza kuiruhusu Kamati yake ya Rufani kusikiliza Rufaa ya mgombea Urais, Michael Richard Wambura- basi hakuna ubaya pia kwa Kamati yake ya Maadili kusikiliza kesi za kimaadili.
Ndumbaro akasema kwa kuwa Malinzi amekataa kesi za kimaadili za Simba kusikilizwa na Kamati ya TFF, wao (Kamati ya Uchaguzi ya Simba) watazipeleka Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Na jana, Mwenyekiti wa Simba SC anayemaliza muda wake, Alhaj Ismail Aden Rage amesema kwamba, uchaguzi wa klabu hiyo upo pale pale kama ulivyopangwa Juni 29, mwaka huu kwa sababu si yeye wala TFF mwenye uwezo wa kutengua hilo kwa sasa.
Rage ambaye pia ni Mbunge wa Tabora Mjini (CCM), amesema kwamba yeye hana mamlaka Kikatiba kwa sasa kubadilisha tarehe ya uchaguzi na TFF pia haiwezi kufanya hivyo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari ya Bunge mjini Dodoma jana, Rage alisema amelazimika kumwandikia barua Malinzi ili kuinusuru klabu hiyo iliyokumbwa na migogoro kwa takriban miaka miwili sasa.
“Juni 15 mwaka huu nilipokea barua kutoka kwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi akinitaka utekelezaji wa mambo matatu; kwanza kuunda kamati ya maadili, kusimamisha mchakato wa uchaguzi mkuu wa Simba na mwisho kuhakikisha maagizo hayo yawe yamekamilika kufikia Juni 30 mwaka huu,” amesema Rage.
“Klabu ya Simba ni muhimu sana katika maisha yangu, nimeichezea na kuitumikia kama Katibu Mkuu 1982 na nimeingia katika kumbukumbu muhimu kwa kuwa Rais wa kwanza wa klabu hii.
“Kwa kutambua hilo, leo nimemwandikia barua Malinzi kumuomba asisitishe uchaguzi wetu, aache ufanyike Juni 29 kama iilivyopangwa. Ninatambua anayo mamlaka ya kuweza kuuchelewesha.
“Usajili (wa wachezaji) umeanza tangu Juni 15 mwaka huu, kusitisha uchaguzi ni kutoitendea haki klabu ya Simba kwa sababu mimi na uongozi wote unaomaliza muda wake tumezuia usajili hadi pale viongozi wapya watakapopatikana,” amesema zaidi Rage.
Kuhusu kuunda kamati ya maadili, Rage amesema masuala mengi ya kimaadili yanayowakabili baadhi ya wagombea akiwamo Michael Wambura aliyeenguliwa katika kinyang’anyiro cha Urais, yako juu ya uwezo wa klabu ya Simba, hivyo anayarudisha TFF.
“Wambura anakabiliwa na makosa ya enzi za FAT (Chama cha Soka Tanzania – sasa TFF), Simba haina mamlaka ya kuyasikiliza, hivyo nimeyarudisha kwa Malinzi kule TFF,” amesema Rage.
Katika mtiririko huu, ina maana tunasubiri majibu ya Malinzi baada ya kuwasikia, kuwasoma Ndumbaro na Rage.
Katikati ya Ndumbaro na Rage kuzungumza, wanachama wa klabu hiyo pia waliandamana hadi makao makuu ya klabu, Mtaa wa Msimbazi juzi na kumsihi Malinzi awaache wafanye uchaguzi.
Kama alivyosema Rage, dirisha la usajili wa wachezaji linatarajiwa kufungwa Juni 30 na tangu limefunguliwa Simba SC imekuwa katika mgogoro wa uchaguzi.
Hivyo mpenzi yeyote wa dhati wa Simba SC kwa sasa atapenda kuona klabu yake inapata viongozi wapya, wanaingia ofisini kwanza kujenga timu ya kucheza Ligi Kuu msimu ujao.
Simba SC wamepitia katika misimu miwili mibovu wakiboronga na kushindwa japo kupata tiketi ya kucheza michuano ya Afrika.
Wazi, baada ya kipindi hicho kigumu, wanachama na wapenzi wa klabu hiyo watahitaji kuona Simba SC inarudisha heshima yake msimu ujao.
Na ili waweze kuweka mikakati ya kurejesha heshima msimu ujao, lazima wafanye uchaguzi wao mapema kama walivyopanga, viongozi wapya waingie ofisini kuanza kukimbizana katika usajili.
Inafahamika wazi kwamba mizengwe yote hii inatokana na Wambura, ambaye Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC ilimuengua kwa sababu alikiuka Katiba kwa kuipeleka klabu hiyo Mahakamani, jambo ambalo FIFA inakataza.
Wambura alikata rufaa, Kamati ya Rufani ya TFF chini ya Mwenyekiti Wakili Julius Lugaziya, ambako alishinda na kurejeshwa kwenye kinyang’anyiro. Wakili Lugaziya alisema Kamati yake iliamua kumrejesha Wambura kwa sababu baada ya kosa alilolifanya aliendelea kuhudhuria mikutano ya klabu, kulipia ada zake za uanachama na pia akateuliwa katika Kamati ya Utendaji, iliyounda Kamati ya Uchaguzi ya sasa chini ya Ndumbaro.
Lakini juzi, Ndumbaro baada ya ripoti ya Wakili Lugayiza alisema amemuengua tena Wambura kwa sababu amekiuka kanuni za uchaguzi kwa kufanya kampeni kabla ya muda
“Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC ilijadili kuhusu vitendo vya wagombea kupiga kampeni kabla ya muda wa kampeni ulioruhusiwa. Kwa mujibu wa Mchakato wa Uchaguzi ya Simba Sports Club, muda wa kampeni unaanza tarehe 24 -28 Juni 2014,”. “Hapo awali kamati ilibaini kuwa wagombea wawili wa nafasi ya urais; Michael Richard Wambura na Evans Aveva walifanya vitendo vya kampeni siku ya kuchukua na kurejesha fomu za kugombea. Tarehe 25 Mei 2014, Kamati iliwapa ONYO KALI la maandishi wagombea hao na kuwataarifu kuwa hatua kali zaidi zitachukuliwa dhidi yao, ikiwemo kuondolewa katika kinyang’anyiro cha uchaguzi,”.
“Baada ya Kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club kumuondoa Bw. Michael Richard Wambura katika kinyang’anyiro cha uchaguzi Mkuu wa SImba SC, Bw. Wambura aliitisha Mkutano na waandishi wa habari, aliitukana Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC na kutoa matamshi ambayo ni Kampeni,”.
“Baada ya ya Kamati ya Rufaa ya uchaguzi ya TFF kumrejesha Bw. Wambura katika Kinyang’anyiro cha Uchaguzi Mkuu wa Simba, Bw. Wambura aliitisha tena mkutano wa waandishi wa habari, aliisifu kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF, kwa mara kwanza aliisifu Kamati ya Uchaguzi ya Simba SC na kutoa matamshi ambayo ni wazi kuwa ni kampeni. Baadhi ya Matamshi aliyoyatoa kupitia vyombo vya habari ni kama ifuatavyo: “Simba Sports Club inahitaji zaidi wadhamini na sio wafadhili. Wafadhili kazi yao in kutoa fedha mfuko wa kushoto na kuepeleka mfuko wa kulia. Simba ilikuwa na viwanja vitatu lakini kimoja kimeuzwa na wajanja na vimebaki viwili tu,”.
“Kamati ya Uchaguzi ya Simba ilitafakari matamshi hayo, na kubaini kuwa hiyo ni kampeni ya waziwazi wakati muda wa kampeni bado haujaanza. Kamati ya Uchaguzi ya Simba ililipa jambo ili uzito wa kipekee kwa sababu Mkosaji amekuwa na tabia ya kurudia kosa hilo hata baada ya kupewe onyo la maandishi,”.
“HIVYO BASI: Kwa mujibu wa mamlaka ya kikanuni, hususan Ibara za: 6 (1) (a) – (g); 6 (1) (L) na 14(3) za Kanuni za uchaguzi za TFF – 2013, Bw. Michael Richard Wambura anaondolewa katika kinyang’anyiro cha uchaguzi wa Simba SC, 2013, kwa kosa la kurudia kufanya kampeni kabla ya muda wa kampeni ambao umepengwa,”alisema Ndumbaro.
Zipo imani kwamba Wambura ni sahiba wa Malinzi na vurugu zote hizi ni kwa sababu anataka kumbeba katika uchaguzi huo.
Suala hili linaweza kuwa na mlolongo mrefu iwapo litakuzwa kwa kutaka kufikishana FIFA, lakini matokeo yake, Simba SC ndiyo itaathirika.
Baada ya Wambura kuruhusiwa kimakosa kulipia ada zake za uanachama, kushiriki mikutano na hata kuteuliwa katika Kamati ya Utendaji, haitakuwa vyema kosa lingine likafanyika kwa kumruhusu agombee na uongozi wa klabu.
Lakini kitu kizuri zaidi kwa sasa ni kuiacha Simba SC ifanye uchaguzi wake kama ilivyopangwa Juni 29, ili iweze kujipanga kwa ajili ya Ligi Kuu msimu ujao. Hayo mengine, yatafuatia.

.png)
0 comments:
Post a Comment