• HABARI MPYA

  Jumatatu, Juni 23, 2014

  YANGA SC YASAJILI WAKALI WAWILI KIKOSI CHA NOOIJ, BARTHEZ AONGEZEWA MKATABA, SIMBA WALIE TU

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  YANGA SC imekamilisha usajili wa wawili wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars chini ya kocha Mholanzi Mart Nooij,  BIN ZUBEIRY imeipata hiyo.
  Habari zisizo na shaka, ambazo BIN ZUBEIRY imezipata kutoka Yanga ni kwamba wachezaji waliosajiliwa ni beki Pato Ngonyani na kiungo mkabaji, Said Juma.
  Aidha, Yanga SC pia imesajili mchezaji wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Saleh Abdallah. Ngonyani anayecheza kushoto na nafasi zote za kati, amesaini Mkataba wa miaka mitatu, wakati Said Juma amesaini miaka miwili na Saleh Abdallah amesaini miaka mitatu pia.
  Yanga imesajili wawili kikosi cha Taifa Stars

  Aidha, Yanga SC imewaongezea mikataba wachezaji wake Jerry Tegete, Said Bahanuzi, Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Ally Mustafa ‘Barthez’ ambao wote wamesaini miaka miwili kila mmoja.
  Yanga SC imesitisha mpango wa kumtema kiungo Nizar Khalfan ambaye amebakiza mwaka mmoja, wakati kipa kipa Yusuph Abdul, mabeki David Luhende, Ibrahim Job, viungo Athuman Idd 'Chuji', Geroge Banda, Rehani Kibingu, Hamisi Thabiti, Bakari Masoud, Abdalllah Mguhi ‘Messi’ na washambuliaji Reliants Lusajo na Shaaban Kondo wameachwa.
  Yanga SC sasa imekamilisha usajili wa wachezaji wa ndani na sasa inataka kuongeza mchezaji mmoja wa kigeni.
  “Tunamsubiri kocha mpya akifika akaiona timu, atashauri zaidi, ila sisi tunafanya mambo yetu kimya kimya, hatuna mbwembwe, ila mwisho wa siku tutakutana uwanjani,”kimesema chanzo kutoka Yanga SC.
  Simba SC ilikuwa ina mpango wa kumrudisha kipa wake Ally Mustafa ‘Barthez’ na kwa kuongeza mkataba Jangwani, maana yake Wekundu wa Msimbazi ‘wamekula za uso’.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC YASAJILI WAKALI WAWILI KIKOSI CHA NOOIJ, BARTHEZ AONGEZEWA MKATABA, SIMBA WALIE TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top