• HABARI MPYA

    Saturday, June 21, 2014

    UFARANSA HIYOOO 16 BORA KOMBE LA DUNIA JAPO BENZEMA ALIKOSA PENALTI

    UFARANSA imejihakikishia kiting 16 Bora ya Kombe la dunia baada ya kuichapa mabao 5-2 Uswisi katika mchezo wa Kundi E usiku huu mjini Salvador.
    Mabao ya mabingwa hao wa 1998 yamefungwa na Olivier Giroud, Blaise Matuidi, Mathieu Valbuena, Karim Benzema na Moussa Sissoko.  
    Kikosi cha Didier Deschamps kilichofuzu kwa mbinde Kombe la Dunia, kingeondoka na ushindi mnene zaidi kama Benzema asingepoteza mkwaju wa penalti, baada ya yeye mwenyewe kuangushwa na Stefan Lichtsteiner.  
    Heshima: Karim Benzema akishangilia baada ya kuifungia Ufaransa bao la tatu katika ushindi wa 5-2 dhidi ya Uswisi


    Ufaransa sasa imetimiza pointi sita baada ya kucheza mechi mbili, ikifuatiwa na Uswisi yenye pointi tatu wakati Ecuador na Honduras zinazomenyana hivi sasa zote hazina pointi.
    Kikosi cha Ufaransa kilikuwa; Lloris, Debuchy, Varane, Sakho/Koscielny dk66, Evra, Sissoko, Cabaye, Matuidi, Valbuena/Griezmann dk82, Giroud/Pogba dk63 na Benzema.
    Uswisi; Benaglio, Lichtsteiner, Djourou, Von Bergen/Senderos dk4, Rodriguez, Inler, Behrami/Dzemaili dk46, Mehmedi, Xhaka, Shaqiri na Seferovic/Drmic dk69.
    Tripped: Real Madrid front man Benzema is brought down by Stefan Lichtsteiner in the corner of the penalty area
    Mshambuliaji wa Real Madrid, Benzema akiangushwa chini na Stefan Lichtsteiner, lakini picha ya chini inamuonyesha akikosa penalti aliyoitengeza mwenyewePicked it: Benaglio goes the right way to save Benzema's spot-kick
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UFARANSA HIYOOO 16 BORA KOMBE LA DUNIA JAPO BENZEMA ALIKOSA PENALTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top