• HABARI MPYA

  Jumatatu, Juni 23, 2014

  KASEJA AULA YANGA SC, KUENDELEA KPIGA KAZI JANGWANI HADI 2015

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIPA Juma Kaseja ataendelea kuchezea Yanga SC kumalizia Mkataba wake wa mwaka mmoja, imeelezwa.
  Habari za ndani kutoka Yanga SC, ambazo BIN ZUBEIRY imezipata zimesema kwamba Kaseja hataachwa kama ilivyokuwa imevumishwa awali.
  “Juma Kaseja na Ally Mustafa Barthez wote wanabaki Yanga SC,”kimesema chanzo.
  Anabaki; Juma Kaseja ataendelea kupiga kazi Yanga hadi msimu ujao

  Mwishoni mwa msimu, kulikuwa kuna habari kwamba Kaseja ataachwa kwa sababu ameshuka kiwango kutokana na kufungwa mabao rahisi katika mechi kadhaa. 
  Kaseja sasa atabakia kwenye kikosi cha Yanga SC na makipa wote aliowahi kudaka nao Simba SC, Barthez na Deo Munishi ‘Dida’.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KASEJA AULA YANGA SC, KUENDELEA KPIGA KAZI JANGWANI HADI 2015 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top