• HABARI MPYA

  Jumatano, Juni 25, 2014

  NIGERIA YAITOA KIMASOMASO AFRIKA, YATINGA 16 BORA KOMBE LA DUNIA

  NIGERIA imeitoa kimasomaso Afrika baada ya kufuzu hatua ya 16 Bora ya Kombe ka Dunia, licha ya kufungwa mabao 3-2 na Argentina katika mchezo wa Kundi F uliofanyika Uwanja wa Beira-Rio mjini Porto Alegre, Brazil.
  Nigeria imemaliza na pointi nne katika nafasi ya pili nyuma ya Argentina yenye pointi tisa, hivyo kuwa timu ya kwanza ya Afrika kufuzu 16 Bora.
  Lionel Messi alianza kuifungia Argentina bao la kwanza dakika ya tatu, lakini Ahmed Mussa akaisawazishia Super Eagles dakika moja baadaye.
  Messi tena akaifungia Argentia bao la pili dakika ya mwisho ya kipindi cha kwanza kabla ya Mussa tena kuisawazishia Nigeria dakika ya ya pili baada ya kipindi cha pili.
  Marcos Rojo aliihakikishia Argentina ushindi wa mechi zote za Kundi lake baada ya kufunga bao la tatu dakika ya 50.
  Bosnia imeifunga mabao 3-1 Iran na kumaliza katika nafasi ya tatu kwa pointi hizo tatu, wakati Iran yenye pointi mbili imeshika mkia.  
  Ivory Coast na Cameroon zote tayari zimeaga na timu nyingine za Afrika zenye nafasi ya kwenda Raundi ya pili ni Algeria na Ghana, iwapo zitashinda mechi zao za mwisho. 
  Kikosi cha Argentina kilikuwa; Romero, Zabaleta, Federico Fernandez, Garay, Rojo, Gago, Mascherano, Di Maria, Messi/Alvarez dk19, Higuain/Biglia dk90 na Aguero/Lavezzi dk37. 
  Nigeria; Enyeama, Ambrose, Yobo, Oshaniwa, Omeruo, Odemwingie/Nwofor dk80, Onazi, Mikel, Babatunde/Uchebo dk66, Musa na Emenike.
  Nyota: Lionel Messi (juu) amefunga mabao mawili Argentina ikiifunga Nigeria 3-2 leo
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NIGERIA YAITOA KIMASOMASO AFRIKA, YATINGA 16 BORA KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top